Sponsor

banner image

recent posts

Diamond Hana Pesa, Nimeshakuwa na Wanaume Wenye Pesa-Zari

Diamond Hana Pesa, Nimeshakuwa na Wanaume Wenye Pesa-Zari
Mzazi mwenzake na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Zarinah Hassan ‘Zari’ ameibuka na kumtupia dongo zito mzazi mwenzake huyo na kusema hana pesa.

Zari na Diamond walikuwa kwenye mahusiano kwa miaka minne na walifanikiwa kuzaa Watoto wawili Lakini Penzi Lao liliingia shubiri mapema mwaka jana Baada ya Diamond kuchepuka na Hamisa na kuzaa naye mtoto.


Tangu waachane sio siri Diamond na Zari hawajawahi kuwa na mahusiano mazuri na siku ya Leo ameweka wazi kuwa Diamond hana pesa kama watu wengi wanavyosema.

Zari alifunguka hayo alipoulizwa na shabiki kama Diamond asingekuwa tajiri na maarufu basi Zari asingeweza kuwa naye kwenye mahusiano, Swali ambalo Zari alijibu kuwa Diamond hana pesa.

Siongei haya ili kuonekana na roho mbaya Lakini nimeshawahi kuwa na wanaume wenye pesa nyingi na yeye hayupo kwenye hao watu kwaiyo sikuwa naye Kwajili ya pesa na umaarufu. Wanaume zangu wote niliowahi kutembea nao ni matajiri lakini bado sijapata ambaye hatakuwa anabadilisha wanawake”.
Diamond Hana Pesa, Nimeshakuwa na Wanaume Wenye Pesa-Zari Diamond Hana Pesa, Nimeshakuwa na Wanaume Wenye Pesa-Zari Reviewed by Love Psychologist on May 03, 2019 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.