Sponsor

banner image

recent posts

Najua nakosea, Ila mapenzi yamenizidi nguvu..!!



Kuna Mambo unaweza kuyafanya ukiwa unajua kwa asilimia zote uko wrong lakini kuyaacha unashindwa, Sio muumini wa thread za mapenzi japo ni sehemu ya maisha yangu but nauona kabisa mwisho wangu kwenye mahusiano Sio mzuri hata kidogo.

Mwaka mmoja na nusu uliopita nilipata uhamisho kutoka mkoa wa Mwanza kwenda HQ katika moja ya shirika la umma nililokuwa nafanyia kazi,baada ya kuhamishwa Kuna mtu alitolewa mkoa mwingine katika shirika hilohilo ili aje kuziba nafasi yangu kwa bahati mbaya sikuwa na mawasiliano nae na ilibidi nifanye mchakato wa kupata namba yake ili niweze kumuuzia baadhi ya vitu.

Nikampigia simu rafiki yangu mmoja ili anisaidie namba Kama anayo, nikatumiwa namba lakini namba Sio ambayo niliihitaji baada ya kumpigia yeye alikuwa ni mhasibu ( mwanamke) ambae nae alikuwa amepokea uhamisho wa kuhamishiwa mwanza, nilipowasiliana nae nikaona sie niliekuwa namuhitaji tukapiga stori za kawaida za kikazi tukaishia hapo.

Kesho yake asubuhi nikapokea text ya kunisalimu " nikamjibu" zikaendelea milolongo ya text nyingi ikiwa hatukuwahi kujuana kabla ( japo tulikuwa tunafanya nae shirika moja ila tulikuwa mikoa tofauti, Hivyo sijawahi kumjua Wala kuwasiliana nae hii ndo ilikuwa Mara ya kwanza), ikawa ni kila siku charting za hapa na pale.., but Kuna mda anachomekea text za kimahaba Mimi nikawa najibu Ila sikuwa na mawazo yeyote ya kimahaba kwake kwa sababu hata sikuwahi kumfahamu before, Charting za WhatsApp zikashamiri, Mara tukaanza kurushiana picha ili kufahamiana zaidi, kipindi hicho Mimi nilikuwa 28aged yeye ana 32

Wiki mbili tangu nihamishwe ukatoka waraka serikalini, taasisi na mashirika yake yote yaanze kutumia mfumo wa EPICOR, yakaandaliwa mafunzo juu ya matumizi wa huu mfumo, batch ya kwanza ilikuwa wahasibu Mimi nilihudhuria Kama mtaalam na mchambuzi wa mifumo ya computer kwenye taasisi yangu ikitokea wahasibu na wagavi wamekwama Mimi ndo nakuwa mtu wa kuwapatia msaada. Ile tunaletewa taarifa watu ambao tunatakiwa twende kwenye haya mafunzo huyu dada ( mhasibu )akaanza kuzidisha kuchart na Mimi zaidi ya mwanzo hapa meseji za mapenzi zikawa waziwazi na Mimi nikajitoa ufahamu nikawa naweka chombezo za hapa na pale, maana kwa picha tu alikuwa vizuri balaa japo sikuweza kumtilia maanani Sana kwa sababu aliniambia ameolewa na anawatoto mapacha wawili.

Siku ya jumapili ambayo ndo ilitakiwa tusafiri ili kesho yake jumatatu tuanze mafunzo, alinipigia Sana simu na text nimlipie hotel kwa gharama yangu, mwanzo nilijua anatania ila kadri mda unavyoenda nikajua Yuko serious, kipindi hicho Mimi Niko dar na mafunzo yalikuwa yanafanyika Dodoma, katika chuo kikuu Cha udom, Sasa kila akiniambia nimlipie Mimi nikawa namjibu " usijali nitalipa hotel tutalala wote", nikimtumia hajibu anakaa kimya kwa mda, then ananitext nilipie hotel, namjibu the same.. ananyamaza.

Mida ya mchana kwenye saa7 nikaianza safari yangu kwenda Dodoma tayari kwa mafunzo kwa gari Binafsi, nilimpitia rafiki yangu morogoro ambae nae ni mfanyakazi mwenzangu, tukiwa njiani alikuwa anapiga Sana simu na text kiasi kwamba ilibidi nimuachie rafiki yangu aendeshe ili mimi niweze kuchart nae vizuri, sikutaka kumwambia chochote rafiki yangu na Hivyo hakujua naongea wala nachart na nani.

Mida ya saa2 usiku akanitaarifu ameshafika ila ananisubiri tukale wote, Mara sijisikii vizuri nakusubir ukifika nikuambie kinachonitatiza.., baadae akanitext amepata hotel akanielekeza nikifika nimfuate tukale, nikamjibu haina shida.

Nilipofika Dom nikamwambia rafiki yangu natakiwa niende kwa ndgu zangu usiku huo huo nikamuacha yeye akatafta hotel, nikamfuata alipo huyu dada, nikafika hotel alipo nikapaki gari langu nikampigia simu akawaambia watu wa mapokezi waniruhusu na wanielekeze chumba alipo ( hii ndo ilikuwa Mara yetu ya kwanza kuonana), Ile macho yanamuona tunasalimiana na alikuwa amevaa tight na kitop then kitovu Kiko wazi " yes ameumbika, mweupe wa asili then ana shape iliyobadili akili zangu ghafla nikajikuta dude limesimama, mpaka yeye akagundua kwamba mwanaume tayari Niko wima, akaanza kuleta kuleta stori za kiromantic, unajua wewe unafanania na IT kabisa Wala hukukosea kusoma hayo masuala ya computer, kipindi hicho akili ziko mbali Sana naanza kufikiria zile charting zetu za kimahaba kabla ya kuonana huku najiuliza huyu dada nimuache kweli kwa uzuri wote huu, je atakubali nimle kuonana tu leo nipige mzigo.., maswali yakawa mengi but jinsi ya kumuanza kumuomba mzigo kiserious ikawa shida kwanza tulikuwa hatujazoeana, pili kashaniambia ni mke wa tu.

Baada ya mda akasema anaenda kuoga ni nimsubiri ( bafu na choo ziko humohumo ndani, hii room ilikuwa self, ikabidi niwe mpole) Alivomaliza kuoga akaja kunieleza masuala ya ndoa yake, ndipo nikafahamu kwamba mume wake ni kigogo serikalini na ana pesa but ni mzee wa miaka zaidi ya 54 kwa kipindi hicho.. Akanielezea hata haki yake ya ndoa hamtoshelezi, mwanaume akili akanicheza fasta nikaaanza kujisema " huu utamu lazima niule kwa vyovyote vile", kipindi chote hiki baada ya kutoka kuoga alikuwa na kanga tu moja kafunga chini, nyingine juu..,

Mida ya saa tano usiku akaniambia twende pestana, huko " PESTANA" nilikuwa hata sipafahamu ikanibidi nitoke nje avae, baada ya dk kadhaa akatoka, Alikuwa amependeza balaa seriously nikajikuta naanza kujiambia mwenyewe why Nimetoka hata bila kumkisi, nikaanza kurudisha mawazo yawezekana huyu anahitaji tu urafiki kwangu na ndo maana amekuwa muwazi kwangu kwa kila kitu kinachohusu maisha yake, tulifika pestana nilipapenda Sana ni kiwanja kizuri Sana Cha kula Bata japo kipo nje ya Mji wa Dom, tukaagiza nyama na vinywaji baridi nikamuuliza Kama anatumia pombe akasema hapana, na mm situmii kilevi baada ya kula akaniambia tuondoke japo mm kiwanja kishanikolea mazingira ya kupendeza na DJ alikuwa vizuri kwa stage, sikutaka kumbishia tukaondoka njiani nikamubia inabidi nikatafte hotel nitakayolala akasema twende hotelini kwake Kuna zawadi kasahau kunipa, akinipa ataniruhusu niondoke.

Tumefika room kwake akatoa vipimo vya HIV, akaniambia sorry naomba unipime sikutaka kuuliza maswali nikampima akawa Yuko njema, akaniuliza Kama Niko tayari kupima.., sikuweza kukataa kwa urembo wake, nikajikuta tu nasema " worry out".. nikapima ., Baada ya hapa akanitaja jina langu akasema utalala humu ndani.. Hii ndo ilikuwa siku yangu ya kwanza kuonana nae na kuingia mapenzini na huyu mhasibu.

Ulikuwa usiku mzuri Sana kuutumia na mtoto wa kinyamwezi, kesho yake hatukuweza kwenda kwenye ufunguzi wa mafunzo,na siku yote tukaitumia tukiwa hotelini, ilikuwa ni zaidi ya honeymoon.

Mwaka Jana nilimua kuacha kazi na kufanya Mambo yangu Binafsi niliyoanza kuyaset miaka kadhaa nikiwa kazini, nilipomuelezea nia yangu ya kuacha kazi aliomba ruhusa kazini kunifuata Dsm ili aweze kuongea na Mimi vizuri, alikuja Dsm akakaa kwangu one week akiwa ananisisitizia nisiache kazi japo nilimuambia kwa Sasa nilichohitaji ni kuacha kazi na kufanya Mambo yangu na si vinginevyo, alirudi mkoani akiwa mnyonge, Nilifanikiwa kuacha kazi na kwenda nje ya nchi kwa miezi kadhaa na niliporudi tayari kwa kuendeleza miradi yangu kitu ambacho sikuweza Amini na kilinishangaza ni yet kuchangia 5million katika masuala ya biashara na miradi yangu mwenyew kwa hiaria yake.

penzi letu linakaribia miaka 2 Sasa nadate nae seriously anaonesha kunipenda kupita kiasi na Mimi Kama kaniroga vile najikuta Sina hata mpango wa kumtafta mtu ambae atakuja kuwa mke wangu yaani MTAANI nahit and run ila huyu najikuta ndo nimemuweka kipaumbele, now ananiambia ana mimba na mimba hiyo ni yangu, namuuliza itakuaje ananiambia Wala nisiwaze ameamua kunitunuku mtoto ili hata nikiwa mbali nae awe anafarijika, Cha kushangaza hate usiku wa saa4 Yuko huru kuchart na Mimi.., najiona kabisa Kuna siku balaa lazma linitokee maana Sina uzoefu wa kutembea na wake za watu huyu ndo wakwanza na mahaba anayonipa tunapokuwa sirini utafikiri Mimi ndo niliyetolea mahari.

Najikuta namuwaza Kama mke wangu halali, Kuna kipindi najiuliza hili ndo " LIMBWATA" lenyewe au, nawezaje kumpenda na kumuwazia mke wa mtu namna hii huku najua lazma siku moja hatari inifike.
Najua nakosea, Ila mapenzi yamenizidi nguvu..!! Najua nakosea, Ila mapenzi yamenizidi nguvu..!! Reviewed by Love Psychologist on May 03, 2019 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.