Mbinu za Kumchagua Mwenza Ambaye Hawezi Kukutelekeza
Chagua mtu mwenye msimamo
Muda aliotumia mpenzi wako kudumu katika uhusiano wake uliopita unaweza kukupa ishara ya nguvu ya mtu kudumu na wewe; Unaweza kutumia njia hii kama kipimo cha matarajio ya uhusiano wenu mpya. Ikiwa, kwa mfano, mwenza wako anayetarajiwa alikuwa na mahusiano kadhaa ambayo yalidumu kwa muda mrefu takribani yenye utulivu wa miaka miwili au zaidi, hii inaelezea uwezo wake mzuri wa kujitoa. Kwa upande mwingine, mtu ambaye ana historia ya uhusiano usio thabiti, wa muda mfupi lazima aonekane kama hatari hata kama atatoa kile kinachoonekana kuwa ni sababu za halali. Kamwe haiwezi kuwa kosa la mtu mwingine kila mara anapovunja uhusiano.
Chagua mtu mwenye mfano mzuri:
Kwa mfano, kuchagua mtu kutoka nyumba iliyovunjika, sio aibu. Lakini unaweza kutaka kujua jinsi mtu huyo alivyotatua maumivu hayo. Baadhi ya watu huwa wamejifunza kuwa njia bora ya kutatua tatizo ni kukata tamaa. Tumaini kuwa mtu huyo amejifunza na kutofautisha mambo mengi kutoka kwenye makosa ya wazazi wake na yupo tayari kuonesha matokeo chanya katika maisha yake.
Chagua mtu anayeweza kustahimili msongo wa mawazo:
Watu ambao wanaweza kustahimili matatizo kwa usahihi watakuwa na uwezo zaidi wa kubaki upande wako hata wakati unapopitia mambo magumu. Watu hawa wanaelewa dhana ya kujitolea, uaminifu, na kazi ya pamoja. Watu wenye wasiwasi sana wanaweza kuwa na hofu hasa kwa sababu ya tabia ya kutambua hali yenye shida ambayo ni mbaya sana kuliko ilivyo kawaida.
Chagua mtu mwenye huruma:
Mtu anayeelewa maumivu yako na anayeweza kufanya jitihada za kukuweka sawa pindi unapokuwa katika kipindi kigumu. Chagua mtu mwenye fadhila na mwenye ukarimu; mtu ambaye ana moyo wa huruma, na asiyeogopa kuionesha huruma yake kwa vitendo.
Chagua mtu ambaye haogopi kufunguka:
Amini nakuambia, ni jambo salama sana kuwa na mtu asiye na tabia ya kuyaficha maumivu yake moyoni mwake. Na mojawapo ya hali inayoogopesha zaidi katika mapenzi ni ile hali ya kutoweza kujua anachokiwaza mpenzi wako hasa kuhusu wewe. Watu ambao hawako tayari kueleza kinachowasibu au dukuduku zao hujitengenezea bomu la matatizo bila kujijua, bomu ambalo hata lisipolipuka leo linaweza kulipuka muda wowote siku moja bila hata kujua sababu; unaweza kuwa vizuri sana. Naamini umewahi kusikia mikasa ya watu ambao mapenzi yao yaliisha bila ya wao kutarajia, mume au mke anarejea nyumbani kutoka kazini anakuta mwenza wake amekusanya kilicho chake na kuondoka.
Chagua mtu ambaye anataka kuwa karibu na wewe, kimwili na kihisia:
Chagua mtu anayependa kuwa karibu kihisia na kimwili; mtu ambaye hachoki kuzungushia mkono wake shingoni, begani, kiunoni au kushikilia mkono wako; mtu ambaye anapenda kukubusu. Kugusa kunaweza kuongeza radha yamapenzi katika uhusiano. Na kwa kuchagua mtu ambaye anaonekana kufurahia kuzungumza na wewe. Mtu ambaye hapendi ujisikie mpweke.
Chagua mtu ambaye ana maadili mema na mnayeshabihiana:
Unaweza kupuuzia na kuchukulia kuwa hili ni jambo dogo tena halina maana ya msingi, lakini nakuambia kuwa mtu asiyependezwa na yale unayofurahia anaweza kuishiia kuvuna janga la upweke utakao pelekea kutelekezwa. Na hatimaye wanaweza kumtafuta mtu mwingine ambaye wanaendana naye. Ikiwa wewe ni mkimbiaji, tafuta mkimbiaji; ikiwa wewe ni mwandaaji mziki, tafuta mtu anayevutiwa na muziki; ikiwa wewe ni mtu wa ibada, mtafute mtu anayependa ibada pia!.
Kufuata ushauri wangu sio njia ya uhakika kwamba hamtatengana. Kwa hakika utakuwa na mambo mengine machache ya kuyazingatia kama; kuwa na tabia njema kwa mpenzi wako, kuwa na heshima, na uwe mwepesi wa kutatua matatizo
Usisahau kushare post hii.👍 Share facebook, twitter, Google+ n.k bila kusahau WhatsApp! Share kote wenzio nao wasome
No comments: