Sponsor

banner image

recent posts

Mke wangu ana mahusiano na dereva wa bodaboda, mbaya zaidi anamuhonga pesa zetu za akiba



Habari wakuu.
Mimi ni kijana wa miaka 29 nimeoa mke ana miaka 24 ,tuko kwenye mahusiano kwa miaka mitano sasa tumebarikiwa watoto wawili.

History yangu na huyu mwanamke nilikutana naye akiwa 18yrs. Tulikubaliana tukaoana alinikuta nikiwa vibaya sana financially na timepitia vipindi vigumu mpaka leo hii amenivumilia kwa shida za aina nyingi.

Pia amekuwa kama cornerstone ya mafanikio au maendeleo yangu na kifamilia.amekuwa akinishauri mambo na yanaenda vizuri sana.

Sasa tatizo lilikuja mwisho wa mwezi November nilihisi amekuwa tofauti na kawaida alikuwa bize sana na alijawa na wasiwasi.

Nilianza kufatilia kimyakimya baada ya siku kadhaa nilijua ana mahusiano na dereva wa bodaboda na alikuwa na anamuhonga pesa zetu za akiba,ijulikane mimi huwa nampatia mke wangu pesa asave kwa ajili ya maendeleo ya kifamilia.

This time tulikuwa tunasave kwa ajili kuanza ujenzi mwakani. Niliumia sana nilikaa siku mbili mfululizo bila kumuuliza na bila kula nikiwaza future ya watoto na mustakabali wa familia yangu.

Nilichukua uamuzi wa kumwambia anipe pesa zile bila kumwambia nachofahamu alisita ila alizileta zikiwa pungufu nilimwuliza akaniambia hata yeye hajui anashangaa hela zimeoungua nilishikwa na hasira sana nilimtandika mpaka majirani wakaja kusuluhisha.

Yeye akakimbilia kwa baba mkubwa ambaye alikuwa kama mlezi wetu tuliitwa na kusikilizwa ila nilimweleza ba mkubwa kilichotokea na yeye akabanwa akasema aliongea na huyo bodaboda ila hawajawa na uhusiano yani yupo indenial hakubali makosa moja kwa moja ila mwisho wa kikao tukawa na msimamo mmoja mimi na Baba mkubwa kwamba tuachane.
Ila juzi kabla ya hizi sikukuu mama mkubwa aliniita kisirisiri wakiwa na mke wangu wakanisihi sana tusamehane turudiane ila nilishikilia msimamo uleule naikaondoka ila bado anaendelea kuomba msamaha kupitia mama mkubwa.

Bado nipo dilemma sana wakuu naomba mnisaidie ushauri ukizingatia huyu mwanamke timepitia mambo mengi na changamoto za kimaisha ila moyo wangu nimekuwa mzito sana kumsamehe

NB:Mimi sijawahi mcheat toka niwe kwenye mahusiano nae
Mke wangu ana mahusiano na dereva wa bodaboda, mbaya zaidi anamuhonga pesa zetu za akiba Mke wangu ana mahusiano na dereva wa bodaboda, mbaya zaidi anamuhonga pesa zetu za akiba Reviewed by Love Psychologist on February 25, 2019 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.