Sponsor

banner image

recent posts

Simulizi :Kijana mmoja alikua anataka kuoa....



Kijana mmoja alikua anataka kuoa, alienda kumuambia Mama yake kwani baba yalea alishafariki muda mrefu, Mama yake alimkubalia lakini alimuambia kuwa kabla ya kuoa aachukue likizo ya mweni mmoja na kurudi kijijini kwanza. Kwakua alikua anampenda sana Mama yake alikubali na kuchukua likizo, lakini chakushangaza baada ya kufika kijijini mama yake alimrudisha mjiji, alimpeleka kwa Shangazi yake tumbo moja na marehemu Baba yake, huyo alikua kaolewa na ana maisha mazuri.

Ni muda sana walikua hawajawasiliana kwani ni kama waligombana flani, baada ya Baba yao kufariki ndugu wa Baba yake ni kama waliwatenga ingwa Baba yao ndiyo aliwasomesha na kuwapa kila kitu. Kijana alishangaa lakini Mama yake alimuambia nataka ukae hapa kwa Shangazi yako mwezi mzima ndiyo urudi kwangu. Alikataa lakini mama alialazimishia, Mama yake aliongea na wifi yake na kumuomba akae na mwanae, hata yeye alishangaa lakini kwa aibu alikubali, Mama aliondoka.

Baada ya wiki moja yule kijana alirudi kwa Mama yake, alimuambia Mama nimeshindwa kukaa na Shangazi, manyayaso ni mengi, wananiona kama takataka, mimi naona kama mateso, wanaona kama nimeenda kula kwao wakati mimi nina pesa zangu, siwezi kukaa nao. Mama yake alimuambia lakini wale ni ndugu wa tumbo moja na Baba yako, Kijana alisema hata kama ni bora kubaki hapa kijijini na Mama yangu kuliko kukaa kule mjini ambapo hata hawanijali.

Mama yake alicheka na kumuambia mwanangu unaenda kuoa, una dada zako na una Kaka zako, pia utakua na mke. Nakuona unavyowapenda ndugu zako lakini kumbuka kuwa kaka zako wtaakua na wake zao na dada zako watakua na wauem zao, wote watakua na familia zao na watawajali wenza wao na watoto wao kuliko wanavyowajali wanao. Ukishaoa kama ukifa jua wanao watahangaika na mke wako kama ambavyo mimi nimehangaika na nyie na si Dada zako, hivyo mwanangu kama unanipenda mimi kuliko Shangazi zako basi ukioa mjali zaidi mke wako lakini kama unawapenda Shangazi zako kuliko mimi basi wajali dada zako kwani hao ndiyo Shangazi wa wanao!
Simulizi :Kijana mmoja alikua anataka kuoa.... Simulizi :Kijana mmoja alikua anataka kuoa.... Reviewed by Love Psychologist on February 28, 2019 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.