Mimi ni Mama wa watoto watatu, sijaolewa ila nilikua naishi na mwanaume ambaye aliachana na mke wake miaka kumi iliyopita, nilikutya washacnana na mwanamke ndiyo alimkimbia, ndoa yao ilikua kanisani na kwakua mwanamke alikua antaka mali mwanaume aligoma kabisa kumpa talaka, walipotengana kila mmoja aliendelea na maisha yake. Mimi na huyu mwanaume tulikutana miaka mitano baadaye tukapendana, aliniambia ukweli na hakua na mawasiliano kabisa na huyo mwanamke kwani hawakua hata na mtoto.
Nimezaa watoto watatu na huyu mwanaume, na tumewekeza pamoja vitui vingi, tuna magari mawili ya Biashara pamoja na nyumba moja kubwa tu. Msababu ya kuja kwako Kaka nikwakua, miaka mitatu baada ya kuanza kuishi pamoja na huyu mwanaume na mambo yetu kuanza kwenda vizuri mwanamke wake alianza kujirudi, alianza kumtumia meseji za mapenzi na kumuomba msamaha kwa kumuacha, mwanaume alimpuuzia na kila kitu alikua akinionyesha hivyo tukawa tunamchora tu.
Sikujua kama mimi ndiyo walikua wananichora kwani mwaka jana mwishoni ndipo niligundua kuwa kumbe wamerudiana na mwanamke amejifungua mtoto sasa hivi ana miazi miwili. Nilimuuliza mume wangu hakubisha, aliniambia kuwa alipitiwa na kuniomba msamaha, niliamua kumsamehe lakini tatizo nikuwa baada tu ya kujua kuwa mimi nimefahamu akaanza kufanya mambo kwa uhuru, wanaongea mpaka usiku wa manane, mwanaume kampangia nyumba na anamhudumia kwa kila kitu, siku hizo muda mwingi yuko huko.
Nimekuja kuchunguza nimegundua kuwa anamjengea yule mwanamke na kachukua mkopo kupitia nyumba yetu tulojenga wawili kamfungulia na Biashara. Nilipomuuliza nanijibu kwa sharau kuwa yule ni mke wake na ana mtoto wake, sasa hivi anasema Mama yake kamuambia kuwa ndoa ya kanisani haivunjwi hivyo amsamehe. Nilipomuuliza kuhusu mimi akaniambia mimi hawezi kuniacha kwani bado ananipenda lakni yule mwingine pia hawezi kumuacha kwani wana ndoa ya kanisani, Kaka nimechanganyikiwa sijui nifanye nini.
True Story:Mimi ni Mama wa watoto watatu, sijaolewa ila.....
Reviewed by Love Psychologist
on
February 28, 2019
Rating:
No comments: