USIPOZINGATIA HAYA, HAKUNA CHA MAPENZI WALA NDOA
Habari za Muda huu ndugu wana JF? Leo nawaleta tena hoja nzuri kuhusu vitu vitakavyoweza kukwamisha mahusiano/ndoa yako na njia ya kuondokana nanvyo....Karibu ujielimishe.Unaruhusiwa pia kukosoa.
Wapenzi wengi ambao wamefikia hatua ya kuachana wameshindwa katika vipimo vya kitalaamu kuthibitisha ubaya waliokoseana, ambao unaweza kubeba uamuzi huo mzito wa kuvunja ahadi zao za kimapenzi na hata ndoa.
Kwa mujibu wa watalaam wa masuala ya ndoa na mapenzi inaelezwa kwamba wapenzi wanaoachana huwa hawana sababu za msingi, hii inatokana na ukweli kwamba wanaoachana hawafahamu kiini kilichowatenganisha katika makubaliano muhimu na ya kwanza kabisa ulimwengu ya watu kufikia hatua ya kupeana utu wao.
Inasemwa hivyo kwa sababu ukilinganisha matatizo yanayotenganisha watu hayabebi hoja zinazokubalika na wapenzi wote. Kwa mfano kama wapenzi watasema wameachana kwa sababu wamefunaniana na wakadhani hiyo ni sababu wanakuwa wanaudanganya zaidi umma kwa maana kuna wanaofumaniana, wanaodhalilishana, wanaotukanana, wasioheshimiana kabisa, lakini bado wanadumu katika ndoa zao bila kuachana.
Kwa ulinganifu huo, wachunguzi wa mambo ya ndoa wanasema, kuachana si zao linaloota na kukua kwa siku moja, bali ni migogoro isiyoshughulikiwa kwa muda mrefu ambayo huwaachanisha wanandoa taratibu bila wao kujua.
Kwa maana hiyo wanaoachana au watakaoachana wanatakiwa kufahamu kuwa safari yao ya talaka haianzi na kumalizika kwa siku moja, isipokuwa hufikia katika hitimisho baada ya kuwepo katika mwendo kwa muda mrefu, ambapo dalili zake huwa hizi zifuatazo:
1 : Ikiwa mmeoana na baadaye mkaanza kuonana ni watu msiohitajiana sana katika maisha. (mapenzi kuchuja). Kila mtu anafahamu kuwa wakati wa uchumba mapenzi huwa moto moto lakini baada ya kuoana hujitokeza hali ya kuanza kuzoea. Hii inatokana na ukaribu ambao mwanzo haukuwepo au kusitishwa kwa machimbezo yaliyokuwa yakiboresha uhusiano. Kwa mfano wapenzi wengi wanapokuwa kwenye uchumba hufanyiana mambo mengi yakiwemo ya kutumiana zawadi na kadi au kutoka pamoja kwa matembezi, lakini wakioana hujikuta hawafanyiani hayo, jambo ambalo huathiri mapenzi yao.
Uchunguzi unaonyesha kuwa wapenzi walio kwenye uchumba wanapokuwa pamoja hutumia muda mwingi sana kuongea kwa simu, kutumiana meseji, kuzungumza tofauti na mume na mke. Ukitaka kuthibitisha keti barabarani ukiona mwanaume na mwanamke wamo ndani ya gari hawaishi kucheka na kuzungumza wafuatilie utakuta mwisho wa safari yao wanaagana kila mmoja anakwenda kwake (ina maana si mume na mke hao). Ni nadra sana kuwakuta wanaume wakiwa pamoja na familia zao wakifurahi, jambo ambalo hupunguza upendo na kuleta mazoea na hisia za kutohitajiana sana. Hili halifai likiwepo ni ishara kuwa mapenzi yanakaribia kunyauka.
2 : Mkiwa hamsameheani na kusahau mnapokoseana. Si watu wengi ambao wako tayari kusamehe na kusahau makosa. Wapenzi wa dunia ya leo wakisema nimekusamehe haina maana wamefuta kosa bali hiliweka kando na kulikumbushia wakati mwingine. ‘Hili ni kosa la tatu tarehe fulani ulinifanyia hivi, wiki iliyopita na jana kulinijibu hivi hivi sasa leo siwezi kukuvumilia”
Kauli kama hizi hutoka kwenye vivywa wa watu ambao hawako tayari kusamehe, kosa la mwaka juzi litakumbushwa tena na tena na kuzidi kuchochea ugomvi hata uliokuwa mdogo na kuoneka mkubwa kwa sababu tu umehusishwa na makosa yaliyopita. Inashauriwa kuwa uhai wa mapenzi lazima uambatana na kusameheana kama wanadamu na kusahau makosa. Hili lisipofanyika ni rahisi kuua penzi na kuwafanya watu kuachana. Ni vema kila mmoja wetu akajichunguza tabia yake na kuacha kukumbusha makosa yaliyopita.
3 : Msipokubali kuwekeana mipaka ya kiutawala. Kuna suala linatambulishwa sana siku hizi na wanaharakati, linaitwa usawa wa kijinsia, jambo hili limekuwa likichangia sana migogoro ya ndoa hasa baada ya kutumiwa vibaya na wahusika. Hakuna ubishi mila za kiafrika zinaongozwa na mfumo dume, kuubadili mfumo huu kwa haraka kumekuwa kukiharibu uhusiano mwingi wa kimapenzi kutokana na ukweli kwamba ni wanaume wachache sana ambo wako tayari kuishi na wanawake wanaovutana nao kimamlaka.
Hivyo ili kunusuru hili lisiwe kikwazo katika mapenzi ninashauri kila mwanandoa kuheshimu mipaka yake na kujali zaidi utu na si usawa kama inavyotambulishwa (haya ni mawazo yangu). Watu wanaojali utu katika familia watakuwa tayari kuwapa heshima wanaoishi nao kwa kusikiliza mawazo yao na kutokutumia nguvu kuwakandamiza wengine. Ni vema mwanamke akachungua nafasi yake kwa mumewe na mume naye akamuheshimu mke kwa utu wake.
4 : Msipozungumzia vikwazo vya maisha.
Matarajio ya watu wengi wanapokuingia katika uhusiano wa kimapenzi huwa ni kupata faraja, ni wachache kati yao hufikiria kukutana na vikwazo vya kimaisha. Tafiti zinaonyesha kuwa wakati mtu anapotafuta mpenzi huamini toka moyoni kuwa akiwa na waridi wake matatizo ya upweke, kukosa msaada wa hili na lile yatakwisha lakini baadaye anakuja kubaini kuwa aliyokusudia kuyapata hayapati tena na hivyo kujuta kwa kauli kama hizi. “Kama ningejua kama mwanaume mwenyewe yuko hivi nisingekubali kuolewa.”
Naishia hapa kwa sababau ya muda, ukipata nafasi tembelea Blog yangu utajifunza zaidi masuala mbalilmbali ikiwemo mwendelezo wa somo hili
No comments: