Habari za siku nyingi wadau wangu, baada ya kuwa nje ya Tanzania kwa shughuli zangu za kikazi, hatimaye nimerejea tena nyumbani kuendelea na shughuli za ujenzi wa taifa langu tukufu.
Ukimya wangu ulisababishwa na uwingi wa majukumu yangu, hivyo kwa wale ambao mmekuwa mkiniandikia barua pepe bila kupokea majibu nawaomba mniwie radhi.
Leo nitazungumza kuhusu uchawi ( ulozi ) katika mapenzi . Mmoja kati ya wasomaji wa blogu yangu ameniandikia akiniomba nimuelezee ni dawa zipi ama ni ulozi upi una nguvu sana katika mapenzi ?
Kwa sababu suala hili lina wagusa wengi, nimeona ni vyema nikiandika makala haya ili kuwasaidia na wale ambao hawajapata nafasi ya kuniuliza lakini pengine wangependa kufahamu kuhusu suala hili.
AINA YA DAWA ZA ULOZI WA MAPENZI.
Dawa za Ulozi wa Mapenzi zimegawanyika katika aina mbalimbali kama vile :
i. Dawa Ya Kumvuta Mtu Unaye muhitaji Kimapenzi.
ii. Dawa Ya Kumtuliza Mtu Ambaye Tayari Upo Naye Kimapenzi.
iii. Dawa Ya Kumvuta Na Kumtuliza Mtu Ambaye Upo Naye Kimapenzi lakini anazuzuliwa na mtu mwingine.
iv. Dawa Ya Kumzuia Mke Au Mume Asitoke Nje Ya Mahusiano.
v. Dawa Ya Kumfanya Mke Au Mume Aachane na Mwanaume au Mwanamke Wa Nje.
vi. Dawa Ya Kumfunga Mwanamke au Mwanaume na Kumfanya Asitamani Mtu Wa Nje Au Asitamaniwe na Mtu wa nje na kadhalika.
05. Dawa Iiitwayo “MUTI”: Hii ni moja kati ya dawa zenye nguvu sana katika ulozi wa mapenzi.
Dawa hii inapatikana kwa wingi katika nchi za Togo & Benin ( Dahomey), Nigeria na Burkinafaso. Hapa nchini Tanzania mti huu unapatikana mkoani Tanga katika wilaya za Handeni na Korogwe, wilaya ya Rufiji mkoani Pwani na wilaya za Kasulu na Kibondo mkoani Kigoma.
04. UCHAWI WA KITABU:
Hapa Mtaalamu wa Kisomo Katika
Masuala Ya Sauti na Hewa ( Sound & Air ), atafanya kisomo maalumu
kwa ajili ya kuwaunganisha watu fulani kimapenzi ama kumtuliza mwanamke au mwanaume asiye tulia katika mapenzi.
Uchawi huu una nguvu sana, mtu anaye ishi jijini Dar es salaam anaweza kufanya kisomo na kikamshika mtu anaye ishi Uingereza au Australia.
Katika ulozi huu, mtu anayetaka kufanyiwa uchawi hutakiwa kupeleka majina matatu ya mtu anaye muhitaji.
Majina hayo ni jina la mhusika, jina la baba yake na jina la mama yake mzazi.
Jina la mama ni muhimu sana kwa sababu ndio mzazi ambaye tuna
uhakika na uhalisia wake. Barani Afrika watalaamu wa uhakika wa Kisomo wanapatikana katika nchi za Misri, Algeria, Senegal, Mali, Nigeria na Tanzania.
Nchini Tanzania, wataalamu wa uhakika wa kisomo, wanapatikana Kigoma, Pemba, Lindi, Rufiji na Mtwara katika wilaya ya Mikindani.
03. KUZIKA MNYAMA ( KONDOO) : Huu ni uchawi wenye nguvu sana katika ulozi wa mapenzi. Katika uchawi huu, mtaalamu pamoja na mtu anayetaka kufanyiwa uchawi, hufanya tambiko kwa muda usio pungua dakika arobaini mpaka masaa matatu kulingana na idadi ya kondoo wanao zikwa kisha huchimba kaburi la futi sita na kuzika kondoo akiwa mzima.
Huu ni uchawi wenye nguvu kubwa sana. Nguvu huongezeka maradufu kulingana na idadi ya kondoo walio zikwa kwenye tambiko. Kondoo wakiwa wengi, nguvu ya uchawi nayo huwa kubwa zaidi ya yenye kuogofya na kutisha sana. Huu ni uchawi unaoweza kumfanyia hata mtu ambaye hujamtongoza na akakupenda ghafla na kukufuata yeye mwenyewe na kukun’gan’gania sana.
Uchawi huu huanza kutoa majibu ndani ya siku tatu tu. Kama unataka kumfanyia mtu uchawi huu, nakushauri kwanza uwe na kitu kingine cha ziada kitakachoweza kuwaaminisha watu kuwa mtu huyo hajakupenda kwa sababu ya uchawi, kwa sababu kwa vyovyote vile, ndugu wa mtu aliyefanyiwa uchawi watajua tu kuwa umemfanyia ndugu yao uchawi na bila shaka wataenda kwa waganga au makanisani kwa ajili ya kutafuta suluhisho la tatizo linalo mkabili ndugu yao. Nchini Tanzania, uchawi huu hufanyika sana katika mkoa wa Tabora na Kigoma.
02. USINGA : Usinga ni uchawiama ulozi unaotumika kwa ajili ya
kulinda ndoa na mahusiano ya watu. Watu wengi wanafikiri uchawi huu huitwa TEGO lakini sio kweli, TEGO sio jina la uchawi, isipokuwa TEGO ni aina ya uchawi uliomo ndani ya uchawi uitwao USINGA.
Uchawi wa Usinga ni uchawi wenye nguvu sana, na nikiwa kama
mtaalamu niliye bobea katika masuala ya ulimwengu usioonekana nakushauri kufikiria zaidi ya mara mbili kabla ya kuamua kutumia uchawi wa USINGA.
AINA ZA USINGA :
Kuna aina tano za Usinga, nazo ni kama ifuatavyo :
i. Usinga wa Siafu
ii. Usinga wa Kobe
iii. Usinga wa Remo
iv. Usinga wa Riyama
v. Usinga wa Propola na
vi. Usinga wa Kisu ( Tego )
vii.Usinga wa Mkweche : Usinga wa kumfanya mwanaume anayetembea na mkeo kuwa hanithi katika siku zote za maisha yake.
Sitazungumzia aina zote sita za usinga, ila nitagusia kidogo kuhusu
usinga wa Siafu. Usinga wa Siafu ni usinga wa
hatari sana na mtu aliye tegwa kwa usinga wa siafu anaweza kupoteza maisha yake.
JINSI USINGA WA SIAFU UNAVYO TENGENEZWA.
Usinga wa siafu unatengenezwa kwa kutumia siafu, jogoo aliyekomaa, kitoto cha mbwa ambacho hakina muda mrefu sana toka kizaliwe, mabaki ya mifupa ya maiti iliyozikwa kuanzia miaka ishirini iliyo pita na kuendelea, majani yaliyo kaushwa na mti wa mfausiku, majani yaliyo kaushwa ya mti wa LUFAKALE pamoja na miti mingine kumi na tatu ambayo siwezi kuitaja hapa kwa sababu za ki ethics.
Jogoo aliye komaa huchukuliwa na kuwekwa kwenye kichuguu cha
siafu ambapo sifa watamla na kubakiza mifupa tu. Mifupa ya
jogoo itachukuliwa na kupakwa dawa maalumu kisha itahifadhiwa kwenye tunguli maalumu.
Baada ya hapo, kitachukuliwa kitoto cha mbwa ambacho hakina muda mrefu sana tangu kizaliwe na kuwekwa kwenye kichuguu cha siafu, siafu watakitafuna kimbwa hicho na kubakiza mifupa, kisha mifupa hiyo itachukuliwa na kuhifadhiwa kwenye tunguli maalumu.
Mtaalamu kwa msaada wa jinni liitwalo Munkara ambalo ni jinni la
makaburini ataenda mapangoni au makaburini muda wa saa saba
kamili za usiku na kufanya tambiko maalumu ambapo jinni Munkara litatokea na kumsaidia mtaalamu kupata kipande cha mabaki ya mifupa ya binadamu
aliyefariki kuanzia miaka arobaini iliyopita.
Mtaalamu atachukua mabaki ya mifupa hiyo na kuihifadhi kwenye tunguli maalumu.
MTI WA LUFAKALE : Maana ya LUFAKALE ni ALISHAKUFA TANGU KALE. Lufakale ni mti wenye nguvu za ajabu sana, mbali ya kutumika
kwenye usinga, mti huu hutumiwa na wachawi ili waishi muda mrefu.
Sio kazi rahisi kuyachuma majani ya mti wa Lufakale. Mtu anayeenda kuchuma majani ya mti wa lufakale anatakiwa kwanza ahakikishe upepo hauelekei katika upande aliopo wakati anachuma majani na wala hakuna mtu yoyote
anaye muona.
Akikiuka masharti hayo pamoja na masharti mengine yanayo husiana na kuchuma majani ya mti wa lufakale basi mtu huyo atakufa. Nimetoa maelezo haya ili uone ugumu wa kuchuma majani ya mti wa lufakale. Hivyo basi mtaalamu atachukua vitu vyoe alivyo vihifadhi kwenye tunguli, pamoja na majani ya mti wa mfa usiku, lufakale, miti mingine kumi na moja pamoja na dawa zingine kama saba, na kuviweka kwenye chungu
kisha atakwenda porini usiku wa sita katika eneo ambalo hakuna mtu atakayeweza kumuona kisha atavichoma vitu vyote hivyo kwa pamoja hadi viwe unga unga kisha atauchukua huo unga na kuihifadhi kwenye tunguli
maalumu pamoja na uzi wa usinga kwa muda wa siku saba. Baada ya hapo atautoa usinga, kwa ajili ya matumizi mbalimbali ya kiulozi ikiwemo katika kulinda mahusiano na ndoa za watu.
JINSI USINGA UNAVYO FANYA KAZI :
Kama kuna mtu anamchukua mke wako, basi utachukua usinga
kunuiza na kuutegesha mlangoni kwako, mke wako akisha vuka tu
tayari unakuwa umeshamshika.
Mwanaume atakaye tembea na mke wako, akishamaliza tu kufanya naye tendo la ndoa, atarudi nyumbani kwake vizuri lakini akifika tu mlangoni kwake atadondoka na kuanza kuugua na anaweza hata kupoteza maisha yake.
Mwanaume yoyote yule atakiwa kumsogolea au kumshika mke wako
kwa namna yoyote ile isipokuwa wewe tu.
Hata kama ni mtoto wenu wote atadhurika endapo atamkaribia
mkeo ili mradi tu awe ni wa jinsia ya kiume. Unashauriwa usifanye uchawi huu kama una mtoto mdogo wa kiume.
UTAJUAJE KAMA USINGA UMEMSHIKA MKE WAKO
Ili kujua kama usinga umemshika mke wako, tega kitu chochote cha
chuma, mkeo akikiruka tu hicho kitu kitapasuka. Kitu hicho kikipasuka basi ujue huo usinga umemshika na mwanaume yoyote yule hatomgusa.
Aina % za Uchawi Babkubwa Kwenye Mapenzi...(SOMA TU , USIJARIBU)
Reviewed by Love Psychologist
on
March 09, 2019
Rating:
No comments: