Kwasababu hiyo niliamua kwenda kutafuta mtoto nnje na kweli mwaka huu mwezi watano huyo mwanamke niliyekua natembea naye alipata mimba yangu. Kwasababu hiyo nilijua fika kuwa mke wangu ndiyo tatizo, bila kupanga nilijikuta nakuwa mbali naye, nakua bize na mchepuko na nilianza kufanyia dharau ili aondoke kwani nilitaka kuishi na Mama watoto wangu mtarajiwa lakini mke wangu alivumilia.
Hakuondoka, ilifikia hatua mpaka tukatengana vitanda nampiga lakini alivumilia na mimi sikutaka kumuacha kwani niliogopa mbele ya macho ya watu ntaonekana kama mnyama hivyo nilitaka aniache mwenyewe. Mwezi uliopita mke wangu alikubalia matokeo, aliamua kuondoka, kwakua tulikua na nyumba mbili nilimpa moja ambayo ilikua na jina lake na mimi kubaki na nyumba tuliyokua tukiishi ambayo ina jina langu. Hatukutengana kisheria aliondoka tu na mimi kubaki na Mama mtoto wangu mtarajiwa.
Sasa sababu ya kuja hapa nikuwa, tangu mke wangu kuondoka nilikua sijaonana naye ila wiki iliyopita nilikua nilimsindikiza Mchumba wangu hospitalini nikakutana naye clinic ni mjamzito, nilishangaa na nilipomuuliza aliniambia kuwa ana mimba ya miezi mitatu. Sikua na sababu ya kuuliza kama mimi ndiyo Baba au la kwani najua tuna miezi zaidi ya nane hatujakutana kimwili.
Ana mimba ambayo si yangu, kusema kweli nimechanganyikiwa kwani nawaza kama ana mimba inamaana tatizo si lake labda ni mimi, sas avipi kuhusu huyu mtoto mwingine, je nimrudie mke wangu ili anifichie aibu au nifanye nini? Tangu siku hiyo nimechanganyikiwa, sina raha, namuuliza huyu mwanamke ninayeishi naye anasema mimba ni ya kwangu hakua na mwanaume mwingine, je ni kweli inawezekana ikawa yangu, nimchanganyikiwa nimekua na kisirani mpaka najichukia nachukia kila mtu na sijui nifanye nini?
Anaomba Ushauri...Mimi ni kijana wa miaka 37.....
Reviewed by Love Psychologist
on
March 05, 2019
Rating:
No comments: