Sponsor

banner image

recent posts

Baada ya kunichezea kwa 11 years na kuniacha, sasa nimepanga kulipiza kisasi



Kutoka kwa Mdau


WANAUME SIJUI NI NANI ALIYEWAROGA.

Huyu kaka nilikutana nae wakati nasoma kidato cha pili pale Zanaki nae alikuwa Azania boys.

Tulianza kuzoeana hasa baada ya kuwa tunakutana wakati wote barabarani kuelekea kituoni kwenye kupanda daladala za kuelekea Mwenge wakati huo.

Yeye alikuwa kidato cha 4 na kama unavyojua niliamua kujenga nae urafiki ili iwe rahisi kupata material au 'nondo' za wakati huo.
Urafiki uliendelea na hatimaye yakaanza mapenzi na wakati huo yeye alikuwa form 6 nami niko form 4.
Kama unavyojua mapenzi ya kiuanafunzi, tulianza kuchombezana na hatimaye tukajikuta tunaanza kufanya mapenzi rasmi.
Kiukweli yeye ndie aliyenitoa bikra, hivo sikuwa na mwanaume mwingine nje zaidi yake.
Mapenzi yaliendelea mpaka nikamaliza sekondari, chuo na nikapata kibarua TPA na wakati huo yeye yuko Temeke mwalimu wa sekondari.
Tulijiwekea malengo mengi sana.
Tulikuwa katika mahusiano takribani miaka 8 huku nikiwa najulikana kwao nae wanamjua kwetu.
Sasa balaa lilianza mwaka juzi baada ya kurudi masomoni kusomea u-Afisa elimu wilaya.
Kwanza hakuniambia kama karudi mpaka dada yake aliponiambia kuwa kaka yake amemaliza salama masomo na karudi Dar.
Baada ya kumpigia simu akasema kajisahau.
Ila kadri siku zinavyokwenda naona hakuna dalili ya ndoa wala kuishi pamoja.
Sasa siku kama 4 zilizopita nilimuita sehemu kuongea nae kiunagaubaga ili nijue hatma yangu.
Hapo ndipo akaniweka kila kitu wazi kuwa hawezi endeleza mahusiano nami kwani amepata mtu sahihi na amesema yuko tayari kufidia muda wangu niliopoteza kwake.
Kumbuka kwao na kwetu tulishatambulishana.

Sasa hapa nimekaa na kuwaza jambo moja la kikatili sana (mtanisamehe)
Nina rafiki yangu daktari, nimemuomba anisaidie kupata damu yenye HIV+ ili niweze kumteka huyo kaka, kumchoma na kumuingiza ile damu au kumuomba amuongezee akienda kutibiwa au vyovyote vile afu kila mtu aendelee na maisha yake.
Najua hatagundua maana sijapanga kumfanyia leo wala kesho.

Kanipotezea sana muda.
Tangu nina miaka 17 mpaka leo nina miaka 28 kanipotezea sana muda wangu na wakati wangu.
Almost 11 years leo anakuja kunitamkia haya.
Am so disappointed kwa hili jambo alilonifanyia.
Sina la kumlipa zaidi ya mawazo ya milele ya kukaa na ugonjwa asioujua kaupataje.

Mwanamke akiamua kufanya ukatili hata shetani hukaa pembeni ili ajifunze kutoka kwetu
Baada ya kunichezea kwa 11 years na kuniacha, sasa nimepanga kulipiza kisasi Baada ya kunichezea kwa 11 years na kuniacha, sasa nimepanga kulipiza kisasi Reviewed by Love Psychologist on March 07, 2019 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.