Habari Wadau...
Ni muda mrefu sasa sijachangia humu ndani, majukumu yamenifanya niwe nasoma thread za wenzangu tu.. Ila leo acha niwanasue baadhi ya vijana wanaoelemewa na mizigo mikubwa ya wasaliti bila kujua.
Dalili zifuatazo ni dalili kuu kuwa mwanamke uliyenaye si mwaminifu.
1. Line za simu zaidi ya moja za mtandao mmoja.
Mwanamke mwenye simu iwe moja au mbili, kisha akawa na SIM cards zaidi ya moja za mtandao mmoja, huyo ni MSALITI.
Mfano ana line mbili za tigo, au voda, au airtel, nk.
Ni kawaida ya wanawake wasaliti kutotaka kuwagonganisha wanaume anaotoka nao, hivyo hii mbinu ya line huwasaidia sana.
2. Kukupenda kulikopitiliza.
Hapa nisieleweke vibaya, mwanamke anaweza kukupenda mapenzi ya dhati tu, ila unapaswa uyachunguze. Ukiona mwanamke amewekeza upendo mwingi sana, anajifanya kukujali sana, usibweteke kuwa unapendwa. Hii inaweza kuwa silaha ya kujilinda na madudu yake nyuma ya pazia. Fanya uchunguzi na sio kujisifu kwa wanaume wenzio kuwa unapendwa.
3. Simu kukatwa ghafla katika maongezi.
Kama uko mbali na mpenzi wako, halafu ana kawaida ya kukata simu ghafla kila mara muongeapo kwenye simu, na pengine baada ya hapo akawa hapokei na baadae kukupa visingizio visivyo vya hapa na pale, fanya uchunguzi. Hii ni dalili ya usaliti.
NASISITIZA...Kama simu inakatwakatwa mara kwa mara muongeapo, basi fanya uchunguzi, hii ni dalili ya usaliti.
4. Anakutoa kasoro nyingi sana kila siku.
Mwanamke unapokuwa naye kimapenzi, huwa anaona hakuna mwanaume kama wewe duniani. Lakini unapoanza kuona anatoa kasoro kwa kila ufanyalo, kaa ukijua kuna mtu best zaidi yako ameshakupiku. Fanya uchunguzi!!. Mfano "Hiyo singled veepee?", " Mbona shati kola chafu?", "Leo umevaaje, mbona hujamatch?", "Hiyo simu mbayaa, si ununue nyinginee??" Nk.
5. Anajibu 'very short'
Sio siri bana, wanawake wanapenda sana kuchat na wanaume zao, haswa hawa wasichana wa kidigital. Mwanamke anayejibu "ok", " poa", "sawa", " vizuri" kwa kila swali umuulizalo bila kurudisha swali kwako, huyo ni muongo. Yupo mtu anayemjibu kwa kirefu zaidi. Kuwa makini sana na fanya uchunguzi!!.
6. Anadanganya mbele yako.
Muogope sana mwanamke anayeweza kumwambia uongo mtu mwingine mbele yako. Jua kuwa wewe anakudanganya zaidi ya hivyo. Huyo ni msaliti tu hakuna namna nyingine.
7. Anakwepa sana kukutambulisha kwa rafiki/ndugu zake.
Hili nalo ni jipu, ukiona mwanamke anakwepa sana kukutambulisha kwa rafiki/ndugu zake, jua huyo ameshawatambulisha wengi sana huko. Wewe utamfanya aonekane malaya/hana maana. Chukua tahadhari.!!
8. Ukijiangalia huoni sababu ya yeye kukuganda.
Nikwambie kitu, hakuna mwanamke yeyote duniani ambaye ameumbwa kuwa na mwanaume 'for nothing', NEVER. Kama uko na mwanamke unahisi si wa level yako, na anakupenda sana, pengine anakuhonga wewe huna msaada wowote kwake, huyo yupo hapo kwako kwa 'kazi maalum'. Yupo anayemhudumia. Yupo anayemthamini.. Huenda ukawa wewe ndo unayependwa sana, lakini nakuhakikishia kuwa HAUKO PEKE YAKO.
9. Anajiamini sana katika mambo yake.
Sometimes unamuona kama hahofii sana kukupoteza. Hahofii matokeo mabaya ya jambo mnalotaka kulifanya, hahofii chochote juu yako. Anakuona wewe ni wake tu. Huyu ana mambo mengi sana. Mchunguze!!.
10. Namba nyingi kwenye simu yake 'zimeseviwa' kwa majina ya kike.
Kuwa makini sana katika hili. Kama kila namba inayopiga imeandika 'Cathe, au Joyce, Aisha, Mariam, Sophy, Zai, nk". Kuwa makini sana hapa. Miongoni mwa hayo majina wengine ni wanaume. Fanya uchunguzi. Na pengine huenda ukabahatika kusoma sms kutoka kwa "Joyce" akilalamika kwa nini hapokei simu zake, upofu wa mapenzi ukakufanya uendelee kuamini huyo ni mwanamke mwenzie.. Si kweli. Wanawake huwa hawabembelezani kiasi hicho na wala hawapigiani simu mara nyingi hivyo. Kuwa makini.
Zipo dalili nyingine nyingi. Lakini kwa sasa zielewe na uzifanyie kazi hizi. Kwa hakika utanishukuru baadae.
Dalili 10 za mwanamke msaliti
Reviewed by Love Psychologist
on
March 24, 2019
Rating:
No comments: