Ushawahi kujiuliza kwa nini wanaume wacheshi huwa wamebahatika kupendwa na wanawake wengi?
Imebainika kuwa wanawake hupenda wanaume wacheshi kwa sababu wanawake wanayataka maisha yao yasionekane ya taabu yani wayaone maisha yao yawe ya furaha wakati wote.
Ukiuliza watu ambao wanaujuzi wa kumfanya mwanamke acheke, utaskia wakikuambia kuwa ucheshi ni silaha kuu kwa mwanamke yeyote. Hii ndio unaona wengi wao huwa wanafukuzwa na wanawake wengi.
Vitu unafaa kufanya
Kama wewe hauna uwezo wa kuwa mcheshi usiingiwe na shaka kuwa itakuwa vigumu kwako. Habari njema ni kuwa kuwa mcheshi si lazima uwe na ujuzi wowote ule. Kile ambacho unahitajika ni kufuata mbinu ya uhakika ambayo itamfanya mwanamke yeyote kuweza kutabasamu pindi atakapokuwa na wewe. Kujifunza ujuzi huu wa kumfanya mwanamke acheke si jambo gumu kwako kufanya.
1. Usiwe mtu ambaye anatabirika kwa urahisi
Mtu ambaye anatabirika wakati anapojaribu kufanya ucheshi huwa anaboa sana. Hii inatokea wakati ambapo unapotumia maneno ambayo unayarudia mara kwa mara ana kuingiza maneno ambayo yahapo kwa mada inayozungumziwa. Ukiwa na tabia hii wanawake hawatakuona unaboa pekee bali pia watajaribu kukutenga kwa kuwa wanakuona mtu ambaye hajielewi kimsimamo.
Kile kitu unachohitajika kufanya ni kuhakikisha kuwa kila wakati unamsaprize, yaani uwe na uwezo ambao unakufanya wewe usiweze kutabirika kwa urahisi. Fanya mara kwa mara kujaribu kuja na mambo mengine mapya ambaye yeye hajayatarajia kabisa. Pia unaweza kujaribu kufanya mazoezi ya mambo ambayo unajua bila shaka ukimwambia ataweza kutabasamu ama kucheka.
2. Wakati mwafaka
Hakikisha kuwa timing ya kumchekesha inalingana na sehemu alipo. Kutumia maneno ya ucheshi hulingana na sehemu ambayo mmoja yupo ama hisia ambayo yuko nayo. Usiwahi kutumia ucheshi sehemu ambazo kuna mazishi, sehemu za majanga nk. Pia unaangalia hisia zake kama zinalingana na sehemu alipo. Hakikisha ya kuwa wakati unapomfanyia ucheshi awe na hisia za raha na ya kutaka kuongea.
3. Soma akili yake
Kwa kuwa umekuwa na yeye kwa muda mrefu, utakuwa umefahamu mambo ambayo anayoyapenda na kuyachukia. Hii itakuwa rahisi kwako kutafuta mada ambazo anazipenda halafu unazijeuza na kuzitia nakshi ili ziweze kuleta hisia za ucheshi.
ONYO: Ukiona kama kila wakati unapojaribu kumfanya mwanamke unayemzimia acheke na haufaulu, basi ni ishara ya kuwa kuna dalili kubwa kuwa mwanamke kama huyo hana hisia nyingi na wewe hivyo unahitaji kujaribu kutumia mbinu mbadala ya kumfurahisha
Jinsi Ya Kumfanya Mwanamke Acheke
Reviewed by Love Psychologist
on
March 25, 2019
Rating:
No comments: