Ndoa au mahusiano mengi huvunjika na sababu kuu ikiwa ni waliochumbiana au waliooana baada ya kuishi kwa muda kutambua kuwa wapenzi wao hawana faida katika maisha yao. Hapa Nesi Mapenzi tumekuja na suluhisho hili angalau utambue je huyu unayechumbiana naye amekamilika ama anabahatisha tu.
Zifuatazo ni ishara za kumtambua iwapo mpenzi wako ni perfect.
#1 Mpenzi wako ni msiri. Katika mapenzi mara nyingi siri lazima iwepo kati ya wapenzi wawili. Kuna wapenzi wengine hawajui kuweka siri. Waeza kupata mwanaume ana lalamika kwa Rafiki zake kuwa mpenzi wake si bora kitandani. Jambo kama hili lafaa liwe siri kati yenu. Njia bora ni kukaa nay echini umfunze jinsi gani anaweza kuwa Hodari kitandani badala ya kumuanika na kumsema kwa marafiki zako.
#2 Mpenzi wako hukusaidia. Hapa ndipo penyewe sasa. Katika mapenzi maisha huwa ni kusaidiana. Iwapo mpenzi wako hatoi msaada wowote huyo achana naye. SI msaada wa pesa pekeake bali hata pia msaada wa kimawazo unatakikana katika mapenzi. Tena wapenzi hawafai kuwa mkono nirika. Eeehe! Mpe mpenzi wako zawadi, mtoe dating, mfanyie surprise. Hayo ndio mapenzi.
#3 Mpenzi wako hukutakia mema. Hahahah! Nyie mlio wapenzi je huombeana mema? Si eti wamtakia mpenzi wako mabaya ili umuadhibu. Eti nimemuomba mwanaume wangu pesa akakataa Mungu amjalie agongwe na gari ndio hizo pesa zitumike hospitali tukose wote. Wewe mwanamke ushindwe. Hata kama umenyimwa pesa usimwombee mpenzi wako mabaya kwani hujui pesa alizo nazo zina hesabu gani.
#4 Anatatua ugomvi kivipi. Je mpenzi wako hutumia njia zipi ili ugomvi wenu usifike mbali? Kuna wapenzi ambao huona njia bora ya kusuluhisha ugomvi ni kunyamaziana kwa muda. Hapana. Hii njia huvunja mahusiano kabisa. Njia bora ni kukaa chini muangalie tofauti zenu halafu msuluhishe tatizo lenu wenyewe.
#5 Anakukubali jinsi ulivyo. Enyi wapenzi inapaswa ukubali unyonge wa mpenzi wako na kama ikiwezekana msaidie kwa kumrekebisha. Kunao wanaopendana lakini mmoja kati yao huwa na hasira za haraka, kulalamika bila mpango nk. Matatizo kama haya ni magumu kuyarekebisha. Hivyo basi unapaswa umkubali na ushughulikie tatizo lake polepole na wala usimkemee.
#6 Anakuheshimu. Heshima ni muhimu katika mahusiano. Mahusiano bila hishama hapo hakuna upendo wala mapenzi. Heshimianeni ndio muikuze heshima yenu mpaka ule wakati mtachumbiana. Kama mpenzi wako hakuheshimu basi huyo hakufai. Mtu kama huyo atakuwa nuksi tupu katika maisha yako.
#7 Anakushauri. Utamu wa mapenzi ni kushauriana na wala si kufokeana. Ni vyema mpenzi wako akikukosea akushauri badala ya kukufokea. Hii ni tabia ya wazimu. Dadangu na kakangu usikubali kabisa mpenzi wako akufokee badala yake anapaswa kukushauri. Ushauri wenyewe unapaswa kuwa mwema na wala si mbaya.
Jinsi Ya Kutambua Iwapo Mpenzi Wako Amekamilika
Reviewed by Love Psychologist
on
March 27, 2019
Rating:
No comments: