Sponsor

banner image

recent posts

Kuna tofauti kubwa ya mtu kukuambia nakupenda na mtu kukupenda kweli



Kuna tofauti kubwa ya mtu kukuambia nakupenda na mtu kukupenda kweli. Kusema ni rahisi, kila mtu anaweza kusema na haigharimu chochote ni maneno tu, lakini hupaswi kumuamini mpaka atakapokuonyesha upendo kweli.

Utamsikia mwanamkie analalamika, ananipiga kila siku lakini hatakikuniacha nikimuambia nataka kuondoka anasema nivumilie ananipenda? Je kipigo ni upendo mimi sijui labda huko kwenu ukipigwa ndiyo unaonyeshwa upendo.

Anachepuka, anaipa michepuko yake namba zako ikupigie na kukutukana, lakini ukitaka kuondoka anaomba msamaha na kukuambia nakupenda, nawewe unaringishia kabisa unasema atahangaika kote lakini atarudi kwangu, upendo wake uko kwangu!

Sijui kikwenu, labda lugha yenu ni tofauti na yetu, kwetu akikufanyia hivyo amekudharau, amekuona takataka na wala hakujali, hakupendi, ila kwakua sielewei lugha yenu labda nikweli anakupenda.

Kila siku anakutukana, anakudhalilisha mbele za watu, anatukana ndugu zako na hata Mama yako mzazi, usiku unamvulia nguo na unasema ananipenda lakini anahasira tu. Mimi sijui lugha yenu, ila kikwetu mtu akimtukana Mama yangu, akinidhalilisha mbele za watu basi najua hanipendi.

Hakuhudumii kwa chochote, anakazi nzuri, pesa lakini anakuacha unakufa njaa, unahangaika na watoto unaweka chakula mezani na anakuja kula huku akalewa na tena kwa dharau. Unasema anasema ananipenda bado ila pombe tu ndiyo zimemzidi, Dada yangu, lugha yenu mimi ngumu kuielewa labda kutokujali kwenu ni upendo.

Ana mwezi hatajakutumia hata meseji kusema unaendeleaje, alijua unaumwa umelezwa Hospitalini lakini anakupigia na kutaka uende umpe mechi bila kuuliza hata kama umepona au la. Unamsingizia na kusema ankaupenda lakiini yuko bize na kazi.

Kikwetu labda kama kazi yake ni yakutoa watu roho au kugawa pumzi hivyo hapati muda wa kupumzika ndiyo ningemuelewa. Sisi kikwetu mtu anayekupenda basi haziishi siku mbili bila kukujulia hali.

Nimalizie kwa kusema kuwa, kikwetu hatuangalii mtu anasemaje, mtu anayekupenda anakufanya uwe na furaha, kama upo na mtu anayekuliza kila siku acha upumbavu na kusema ananipenda! Ila na sisistiza sijui kikwenu labda uniambie kulia kwenu ni kucheka!

Hapana wewe nimuathirika tu wa mateso ambaye unaishi na huyo mtu kwakuwa huna namna na umejisahau unajipa moyo kwa kujiambia unapendwa ili uweze kuendelea kuvumilia. Lakini ukweli unaujua kua hakupendi, ila ndiyo hivyo lugha zetu tofauti!
Kuna tofauti kubwa ya mtu kukuambia nakupenda na mtu kukupenda kweli Kuna tofauti kubwa ya mtu kukuambia nakupenda na mtu kukupenda kweli Reviewed by Love Psychologist on March 22, 2019 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.