Sponsor

banner image

recent posts

Kwa Nini Wanawake Wanakataa Kusimama Ukianza Approach Kwao?

Ishawahi kukutokea mara moja au nyingine.

Unajaribu kuapproach mwanamke lakini pindi unapomwita ama kutaka kuchukua atenshen yake ghafla anakupuuza hata kabla hajakwambia jina lake ama kujientroduce vizuri.

Well, hili ni jambo la kawaida ambalo linatokea mara moja au nyingine kwa mwanaume yeyote. Lakini kama hii ndio imekuwa tabia yako ya kuwa kila wakati unapuuzwa na wanawake wakati ambapo unajaribu kuwasimamisha au kuongea nao basi kuna tatizo.


Ok. Unaweza kuwa unajua mbinu zote za kuapproach mwanamke, michongo yote umeihifadhi kwa akili lakini bado kuna kitu unashindwa kukitimiza.

Kitu chenyewe ni kuwa wanaume wengi hukifanya bila wao kufahamu ya kuwa ni makosa makubwa kwa mwanamke....

...kudhani ya kuwa mwanamke atasimama na kuwasikiliza kulingana na maneno wanayoyatoa kutoka kwa vinywa vyao.

Ukweli ni kuwa mwanamke hatosimama kulingana na maneno yako unayoyatoa mara ya kwanza.

Bali hutumia fikra na uingiliaji wa mawazo ambayo ameyajenga kulingana na matukio ya zamani aliyoyapitia.

Jambo ambalo unafaa kufahamu kuhusu wanawake ni kuwa wanajenga uingilianaji wa mawazo ya jinsi ya kuwatizama wanaume kulingana na mahusiano yao ya zamani na wanaume.

Kulingana na wanawake, mwanaume ambaye anajilazimisha kuongea naye, mwanaume ambaye hana thamani katika maisha yake--- kv mwanaume ambaye havutiwi naye-- huwa na tabia moja ambayo wanaonyesha wakati wanapowaaproach....tabia ya kujipaza juu wakati wa kuongea.

Kwa kupunguza maneno mengi ni kuwa wanaume wenye tabia hii kwa kawaida wanapenda kuongea kwa haraka.

(Wanaume wasiokuwa na thamani kwa mwanamke ni wale wanaopenda kuongea kwa haraka kwa kuwa wamezoea kukatizwa katikati wakati wanapoongea ama kupuuzwa na wenzao wanapoongea)

So wewe una hii tabia? Je wewe unajiingiza katika kategoria ambayo wanaonekana kutokuwa na thamani mbele ya wanawake?

Na kama hauna tabia hii mbona unashindwa kuwasimamisha wanawake pindi unapowaaproach?

Well. Uzuri ni kuwa nimekuja na mwongozo na mwongozo wenyewe ni wa haraka ambao nimekuwa nikiusistiza katika machapisho yetu ya awali.

1. Tumia mistari yako pindi unapochukua atenshen yake ya macho
Hii ni rahisi. Pindi ambapo utaiteka atenshen yake kwa kutumia macho anza kutumia mistari yako na michomgo yako bila kusita sita.  Huku kutampa sababu kuu ya kwa nini anafaa kuongea na wewe. 

2. Chukua muda wako wote kuongea na yeye kwa kujivuta
Pindi ambapo utakuwa umeiteka atenshen yake ya macho usiwe na pupa ya kuongea haraka haraka kwani atakupuuza. Chukua muda wako wote wa kuyavuta maneno yako ili kuonyesha ya kuwa huna tamaa.
Mwanzo kuongea kwa mvuto ni moja ya silaha kuu ambayo kila mwanaume anafaa kuwa nayo. 

Upo!? Hizi ni mbinu ambazo ukizitumia vizuri hutakuwa na wasiwasi wa kuwa mwanamke hatosimama wakati ambapo unawaaproach.
Kwa Nini Wanawake Wanakataa Kusimama Ukianza Approach Kwao? Kwa Nini Wanawake Wanakataa Kusimama Ukianza Approach Kwao? Reviewed by Love Psychologist on March 25, 2019 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.