Sponsor

banner image

recent posts

Kwanini Wanawake Wengi Siku Hizi Hawaolewi? Jibu Mubashara Hili Hapa



*KWA NINI WANAWAKE WENGI SIKU HIZI HAWAOLEWI? WENGI HUPISHANA NA WAUME ZAO*

Mwanamke anapigiwa simu kwa namba ngeni, anauliza namba yangu umeitoa wapi? Usiponiambia aliyekupa usinipigie. _HAPO UMEPISHANA NA MUME_

Mwanamke anaingia ndani ya daladala, amekaa na mwanaume, kwa maringo, anachukua earphone na kuweka masikioni na kuwasha mziki ili asiongeleshwe. _HAPO UMEPISHANA NA MUME._

Mwanamke anasalimiwa njiani, anaitikia, akiongeleshwa tena anachuna. _HAPO UMEPISHANA NA MUME._

Mwanamke unatumiwa meseji inbox, hujibu. _HAPO UMEPISHANA NA MUME._

Mwanamke unapigiwa simu na mwanaume, unaona kabisa anakupigia ila hutaki kupokea tu. _HAPO UMEPISHANA NA MUME._

Mwanamke unakwenda gheto kwa mwanaume, una mkoba wako, ukifika muda wa kuondoka unaomba nauli. _HAPO UMEPISHANA NA MUME._

Mwanamke unakwenda kwa mwanaume, badala ya kusonga ugali, cha kwanza unataka chipsi kuku. _HAPO UMEPISHANA NA MUME._

Mwanamke unaanza uhusiano na mwanaume, siku ya pili tu unamwambia bebi sina hela ya vocha. _HAPO UMEPISHANA NA MWANAUME._

Mwanamke upo na mwanaume, anakwambia agiza chochote, bila kujishtukia unaagiza bia. _HAPO UMEPISHANA NA MUME._

Mwanamke unachati na mwanaume, chatting zako ni K, P, Pw. _HAPO UMEPISHANA NA MUME._

Mwanamke unaweka picha mapaja wazi, kifua umebust. _HAPO UMEPISHANA NA MUME._

Mwanamke unamwambia mwanaume akutumie video za ngono kwenye simu. _HAPO UMEPISHANA NA MUME._

_Usilalamike kwamba kwa nini mpaka sasa hivi hujaolewa. Niambie sasa ni mara ngapi umepishana na mume!_
Kwanini Wanawake Wengi Siku Hizi Hawaolewi? Jibu Mubashara Hili Hapa Kwanini Wanawake Wengi Siku Hizi Hawaolewi? Jibu Mubashara Hili Hapa Reviewed by Love Psychologist on March 24, 2019 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.