Madhara ya Kulala Ukiwa Umevaa Sidiria Kwa Mwanamke
Sidiria inavaliwa na mwanamke ili kusaidia kuyashikilia matiti, kuyapunguzia uzito na inasaidia kuongeza kujiamini mbele ya watu. Kwa mara moja inapovaliwa inabadili umbo na muonekano wa matiti, kama kuyainua (kubusti) ili kutengeneza muonekano ambao mwanamke mwenyewe anautaka. Katika miaka ya 1930, muonekano wa kiume kwa mwanamke ilikuwa ndio fasheni inayotamba, kwahiyo sidiria zilivaliwa ili kuficha kabisa maziwa na kuwafanya waonekane kuwa na kifua kama cha mwanaume. Kwa wanawake wenye maumbile makubwa, inawaongezea hali ya kuwa na amani zaidi. Hata hivyo, kumekuwa na mjadala mkali kuhusu madhara ya kuvaa sidiria, hasa wakati wa kulala.
Kutopumzisha matiti
Mara nyingi sidiria huwa zinawaumiza baadhi ya wanawake wanapozivaa wakiwa katika shughuli zao za kila siku, kwahiyo kulala wakiwa pia wamezivaa inaongeza maumivu haya. Wanawake wanaolalia mgongo wanaweza kupata maumivu sehemu ambayo ngozi inagusana na sehemu ya kufungia sidiria na kusababisha kero. Na waya wa upande wa chini wa sidiria unaoshikilia matiti unaweza ukawa na madhara kwa kuchimba sehemu ya chini ya tishu za matiti na kusababisha michubuko au kuvilia kwa damu. Madhara ya matatizo haya yatadumu usiku mzima na kumsababishia mvaaji kero isiyoisha.
Kutotengenezwa tishu zainazoweza kumudu kubeba uzito wa matiti
Ingawa wanawake huvaa sidiria ili kuyasaidia matiti yasizidiwe uzito, inaweza ikasababisha madhara ya kiafya kwa mwanamke. Kwa kuvaa sidiria, matiti yanakuwa hayatengenezi tishu ngumu zitakazouwezesha mwili kumudu kubeba uzito wa matiti. Kwa sababu hii, matiti yatadondoka mapema zaidi kama sidiria itakuwa inavaliwa mara kwa mara. Na kama itakuwa inavaliwa usiku na mchana, matiti hayatapata nafasi ya kutengeneza wala kutumia tishu hizi kabisa, jambo linalolikuza tatizo lenyewe.
Inasababisha Saratani ya matiti
Kitabu cha “Dressed to Kill,” kilichotolewa mwaka 1995, kinasema kwamba sidiria inaathiri uwezo wa mwili kunyonya majimaji, inaongeza joto kwenye matiti na kuathiri kiwango cha protini aina ya prolactin, inayotumika kutengeneza maziwa.
Kwa sababu hiyo, waandishi wa kitabu hicho Singer na Grismaijar wanasema kuwa hali hiyo inaongeza kwa kiasi kikubwa uwezekano wa mwanamke kupata saratani ya matiti. Hata hivyo, Louise Brinton wa Taasisi ya Saratani nchini Marekani anasema kuwa hilo haliwezekani kisayansi kwakuwa haihusiani na kuathiri wingi wa homoni za endogenous, ambazo ndio zinahusiana na kutokea na kukua kwa saratani. Kwahiyo, ingawa wataalamu wanapingana kuhusu hili, watafiti wanaamini kuwa kuvaa sidiria kunaweza sababisha mwanamke kupata kansa ya matiti, na kuvaa kwa muda mrefu kunaongeza hatari hii kwa kiwango kikubwa.
Kutokwa jasho muda mrefu
Kutokwa jasho sana kwa mwanamke mara nyingine ni madhara ya kuvaa sidiria wakati wa kulala. Kitambaa cha ziada kilichetengenezewa sidiria kinazuia mzunguko wa hewa mwilini na kusababisha mwanamke atoke jasho kupita kiasi. Hii inaweza kusababisha muwasho na usumbufu kwa mvaaji. Wanawake wanaona ni lazima walale wakiwa wamevaa sidiria wahakikishe kuwa imetengenezwa kwa kitambaa kinachoiwezesha ngozi kupumua vizuri kama pamba.
Vimbe
Hizi ni vimbe zisizo na uhusiano wowote na saratani (kansa) ya matiti kwa mwanamke. Hizi ni vimbe zinazotokana na mkusanyiko wa tishu zinazoweza kutokea sehemu yoyote mwilini. Dkt. John McDougall akiandika kwenye program yake inayojulikana kama “The McDougall Program for a Healthy Heart” jinsi sidiria inavyoyazuia matiti inasababisha uvimbe kutokea na matiti kuwa na jasho muda mwingi. Hivyo, japokuwa hazina madhara yoyote kiafya, lakini vimbe zinaweza kutokea. Vimbe hizi zinaweza kusababisha ongezeko la hofu kwa mwanamke, na hofu hii ndio yenye madhara kwake.
No comments: