Sponsor

banner image

recent posts

Mimi ni binti wa miaka 27, sijaolewa lakini........



Mimi ni binti wa miaka 27, sijaolewa lakini nina mchumba ambaye nampenda sana, tumekua wkenye mahusiano kwa miaka minne sasa. Sababu ya kuja kwako Kaka si mchumba wangu bali ni Mama yangu mzazi. Baada ya kumuamia kuwa ninataka kuolewa na kumtambulisha mchumba wangu alikubaliana na kila kitu, alifurahi na aliniunga mkono. Kimbembe kilikuja baada ya mchumba wangu kutuma ndugu zake.

Kumbe alikua anafahamiana na Baba yake mdogo na alipomuona alikataa katakata, alianza kuleta maneno maneno kuwa ile familia sio nzuri na mambo mengine mengi. Nilimuuliza sababu za kubadilika ghafla lakini hakutaka kuniambia,a likua akisema tu hataki niolewe na yule mwanaume basi. Mimi nilichunguza na nilipofuatilia nikaja kugundua kuwa Mam yangu mzazi anchepuka, na anatembe ana Baba wa mchumba wangu.

Alipomuona Baba mdogo wa mchumba wangu aligundua kwania likua anamfahamu. Nilichanganyikiwa kwani mapenzi yao bado ni motomoto, nilikasirika na kuamua kumuuliza Mama akaniambia kuwa ni kweli na haiwezekani mimi kuolewa na huyo mchumba wangu kwani itakua ni aibu kwa familia. Mimi nimechanganyikiwa kwekweli, mchumba wangu bado sijamuambia chochote, nawaza kumuacha lakini nashindwa, nawaza nimuambie nini na atanielewaje. Vipi Baba na ndugu wengine nitawaambia ni kwanini naachana na mwanaume ambaye yuko tayari kunioa?
Mimi ni binti wa miaka 27, sijaolewa lakini........ Mimi ni binti wa miaka 27, sijaolewa lakini........ Reviewed by Love Psychologist on March 24, 2019 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.