Habarini Wadau,
Leo nimeamua tu nieleze tukio/ uzoefu mdogo nilioupata katika uhusiano wa Mapenzi wakati nikiwa mdogo kiasi.
Lakini zaidi natamani sisi kama Wanaume tuwathamini sana wanawake wanaoonesha moyo wa kutupenda KWELI na tuthamini upendo wao kwetu.
Ni hivii:
Nakumbuka tangu siku ya kwanza kujoin shule moja maarufu ya sekondari iliyopo Monduli huko Arusha nilikuwa Mtukutu na tangu form One nilikuwa na vikundi vya wanafunzi wahuni kweli tulikuwa tunaita (Mobb) na tuliipa jina kundi letu japo tulikuwa tunafanya vizuri kimasomo, Tulishaapa kutokuwa na uhusiano wa kimapenzi na binti yeyote na kama ikitokea binti akajirahisisha kwetu tunampiga...hiyo ilikuwa kama kauli mbiu na tuliona huo ndio Uanaume Haswaa!
Kila jumatatu ilikuwa ni siku rasmi ya kuimba wimbo wa Taifa na wa Shule kwa adabu, kupandisha Bendera ya Taifa na kukaguliwa usafi wa mwili na mavazi.
◆ Sasa nakumbuka jumatatu moja asubuhi tunatoka kwenye Parade tunaelekea darasani nikawa naongozana na binti mmoja mgeni bila kujua anakuja darasani kwetu.
Mara ghafla nikashangaa palepale ninapokaa katika siti yangu akaja kukaa yule binti, na kiukweli alikuwa mzuri ila sikutaka anizoee. Aisee alikuwa yuko sharp kujibu maswali na kimombo kilikuwa kinapanda kwsbb kalitoka English Medium school huko Dsm wakati sisi ni wa St. Kayumba. Kiukweli ile hali ilikuwa inaniboa sana nilimwona ana kiherehere sana...japo alikuwa ananiokoa na fimbo sometimes kwa kunisaidia masomo darasani.
Nilikuwa kila nikienda Bwenini wenzangu wananiambia " Naona umeletewa mrembo, bibie mlainii " aisee kweli hisia hazifichiki, kumbe Hellen alinipenda sana japo nilikuwa rafu mno hadi kimavazi. siku zilivyozidi kwenda nikaanza kuona umuhimu wa yule binti haswa tulivyoingia form 2 kuelekea 3, alikuwa ananisaidia kwa vingi mno japo sikujali na nilikuwa namsema vibaya kwa wenzangu.
● Kwa Mfano, vitu ninavyokumbuka kutoka kwake :~
Tulikuwa na ratiba ya kuchunga ng'ombe za shule kila jumamosi kwa form One wavulana, ikifika zamu yangu alikuwa anafua nguo zake mapema then anakuja kushinda na mimi katika kuchunga bila kujali hadi jioni napoenda kuchukua nusu lita yangu ya maziwa kama kawaida.
Nakumbuka siku ile alipoenda kuchukua kitabu cha nyimbo cha kilutheri, wakati huo kikiitwa "MWIMBIENI BWANA" cha mama yake akafuta jina la mama yake kwenye kitabu na Biblia akajaladia na kunipa mimi ili nisiadhibiwe na Mwl. wa UKWATA kwa kupoteza hivyo vitabu.
Nakumbuka Visiting days, alikuwa akitembelewa na wazazi wake na gari binafsi kutokea Dsm ananiita mimi na rafiki yake mmoja wa kike nawasalimia wazazi wake...na baadae jioni ananigawia kuku, viepe, juice na matunda ya kutosha napata na kupeleka Dom kisha tunatumia na wenzangu ila bado namsema vibaya kwa wenzangu (lakini moyoni nimeanza kumpenda haswa Hellen)
Nakumbuka jumapili tunaenda kanisani KKKT Monduli mjini, kisha tukirudi tunakaa uwanja wa mpira karibu na goli flani hata mpaka jioni...mara nyingine ananiegemea mpaka anasinzia mtoto wa watu...huku ameleta juice ya Fruto ile ya manjano na biskuti za Marie tunakula.
Nakumbuka alimwambia mama yake "Tukimaliza shule tutaoana na.........(mimi)"
Kwakweli alikuwa ananihadithia habari za kuchekesha za nyumbani kwao zoote kuhusu Wazazi wake, mdogo wake hadi dereva wao aliyekuwaga anakuja na wazazi wake shuleni na ambaye hadi mimi jamaa alinizoea sana na kunipenda hadi jina namkumbuka (Misana) tall hivi ni Msukuma.
■ KUHUSU SUMMER SEASON:
Kulikuwa na Wazungu wanakuja kiila mwaka pale shuleni kutoka USA, Denmark na Sweden na wanawachagua wale wanafunzi brighter zaidi na kuishi nao na kufanya nao tour za mara kwa mara na baadae wengine wanaenda aidha USA, Denmark au Sweden...Hellen nae akachaguliwa kwajili ya lugha na performance darasani.
Siku moja wazungu wawili ambao walikuwa wapenzi wakatuona kila mahali nipo na Hellen mmoja akasema wao akasema
" These two will marry each other "
Kuna masweta mazuri na mazito yalikuwa yanaletwa na hao wazungu yameandikwa "Power to the Bauer" la Hellen nikachukua nikawa navaa mimi...na akiniona nimevaa anafurahi mno. LAKINI, Kumbuka hapo bado nikiwa na wenzangu natalk shit kwake japo simwambii lakini huku naumia moyoni kumsema vibaya.
■ NISICHOKISAHAU KAMWE ■
Mwezi April tukikaribia kufunga shule kwajili ya Pasaka, Hellen alikuwa ananiambia anataka kupajua kwetu Arusha, kabla hajaenda kwao kwsbb kuna shangazi yake anaishi Sakina Arusha, hivyo atawaambia wazazi wake kuwa atabaki kwa Aunt yake...Sikumjibu chochote zaidi ya kumwangalia tu kwsbb nilikuwa na wenzangu na sikutaka kuonesha kuwa namjali. Najua aliumia kweli na hata mimi niliumia sanaaa.
Akaja tena kuniambia basi nipaki mizigo yangu halafu watanipeleka mpaka Arusha mjini waniache mimi wao waendelee na safari hadi Dsm tena akaniambia wazazi wake hawana shida yeye atawaambia nikamkatalia akachukia tena.
Siku ya Alhamisi kuamkia ijumaa siku ya kufunga shule nakumbuka akachukua daftari langu jipya halafu nyuma ya daftari akachora picha ya Bwana harusi na Bibi harusi akaandika majina yetu.
Chini akaandika wimbo wa ROXETTE
It Must have been in Love" ......but its over now.
Nikamuuliza kwanini anaupenda huo wimbo akaniambia tu yeye na dada yake wanaupenda sana. Baas
■ BAADA YA KUFUNGUA SHULE
Nakumbuka kwenye jumatatu au jumanne, tukiwa kwenye groups tunachambuliwa kitabu cha "No Longer at Ease" na Mwl. Madam Mbise (maarufu kama May Be) hiyo ni form three...mwalimu wakati anamalizia ili aondoke akatuambia tu straight away kuwa Halafu kuna mmoja wenu amefiwa na wazazi wake wote wawili na yeye ameumia sana pia. Wanafunzi kimyaaa tukaanza kuangalia ni kina nani bado hawajarudi.
Ghafla akasema ni mwenzenu Hellena. Mimi moja kwa moja nikamwomba mwalimu ruhusa ya kwenda nje kujisaidia. KWAKWELI kidogo nianguke, nikapata kama tumbo la kuhara na kuhisi kama sipo shuleni kabisa.
Wakati wa break nilienda Dom aisee nililia Mnoo sio siri siku nzima.
Mara nikaanza kukumbuka nilivyokuwa namjibu, pembeni nikaona hotpot flan hivi nzuri inayofanana na yake na alinipa kama zawadi ya kuwekea msosi nikakumbuka mengi.
Nilikumbuka mengi sanaa mazuri aliyonifanyia na kujiuliza kwanini mimi sikumjali au kuonesha kumpenda.
Baadae, tukasikia tu kuna waalimu wawili wanaenda kutoa pole msibani kumbe ni kweli Hellen na wazazi wake pamoja na dereva wao walipata ajali Tegeta Dsm wakafa pale pale kasoro dereva wao (Misana) akaja kufa baadae kabisa kwa kuishiwa damu.
Sikuwahi kufika Dsm hata siku moja na nilitamani pangekuwa ni karibu ili nikamwone tu lakini haikuwezekana.
● UJUMBE:
Ukibahatika kumpata mtu anayekupenda kweli, onesha kumjali au kujali hisia zake kwasababu hujui nini kitatokea mbeleni.
MKASA MZITO: Kamwe sintasahau Ijumaa 13th April 2001.
Reviewed by Love Psychologist
on
March 24, 2019
Rating:
No comments: