Mke wangu alivojikuta anavuruga ndoa yetu akijua anaimarisha ndoa yetu...
Nikiwa baba wa familia ya watoto watatu,na mke mmoja niliyejaaaliwa na mwenyezi Mungu kumpata hakika sikuwahi kujutia kumchagua katika wengi niliowahi kuwaona,ilikuwa ni ndoa yenye furaha na amani tele japo mapungufu hayakosi lakini ni machache tena yenye kuvumilika..
Nikiwa naendelea na majukumu yangu kama baba wa familia kuhaangaika huku na kule ili hali familia yangu ipate mahitaji yote ya msingi lakini hali ikawa tofauti kwa mie wangu,nini kilijli songa nayoo.....
Baada ya heka heka za huku na kule mara nipo mikoa tofauti kikazi na mda mwingine kurudi usiku Kutoka Kazini hapa najua mliowahi kufanya kazi private sector mtaelewa.mke wangu aliweka kichwani mwake kuwa tayari nina wanawake wengine hali iliyompekea kuanza kunifatilia bila mafanikio yoyote,ilifika kipindi akatafta kampani Kutoka sehemu mbali mbali Kazini kwake na kanisani tulipokuwa tunasali,
Baada ya mda mfupi nikapata tatizo la kuugua ilibidi niwe nyumbani kwa mda wa Mwezi mzima nikiwa napata Matibabu,katika kipindi chote nikiwa naumwammke wangu alikuwa bize kuongeza na wacghungaji na wazee wa kanisa bila mimi kujua chochote,Mungu ni mwema hali yangu iliendelea vizuri na nikapona kabisa,mke wangu alianza kunisihi sana kuhusu kuhudhuria ibaada kila jumapili nami nikimwambia nitaenda tu kanisani hakuna tatizo...
Ilipita mda kama wiki mbili sijaitikia agizo la mke wangu kwenda kanisani,kumbe mda wote ule walikuwa wamesha kaa kikao mke wangu,Mchungaji na wazee wa kanisa kuwa nikijitokeza tu kanisani inabidi nitangaziwe dhambi ya uzinzi mbele ya kanisa na nitengwe pale pale...
Baada ya kuona sijaitikia mke wangu alizi kupata wasi wasi wa kuwa pengine dili hilo mimi ninalijua,ikiwa ni jumapili iliyo tulia kabisa tena iliyoniinua kitandani mapema nijiandae kwenda kanisani huku na watoto wetu wakiwepo nyumbani siku hiyo ghafra nikasikia moyo wangu unagoma kabisa kwenda...niliishia kuoga nikapaka mafuta na kurudi chumbani kuendelea kulala..
Ni siku ambayo mke wangu alipanga na viongozi kunidhalilisha mbele yamkanisa either niwepo au nisiwepo...
Wakiwepo watoto,ndugu jamaa na marafiki ndani ya kanisa ghafra Mchungaji akamkaribisha mke wangu mbele ya kanisa na kuanza kusema Mme wangu anazini na anamke mwingine naomba kanisa limtenge,wachunga wakaitikia na kusema ni Kweli wameletewa kesi kama hiyo na mke wangu na ndivo ilivo leo ndiyo siku ya kumtenga Bwana x..
Kanisa lilipigwa butwaa na mshangao kwa kile alichoinuka na kusema mke wangu mbele ya kanisa akiwa amebeba degree yake kichwani mwake.
Mwanamme nikajisemea yote yatapita chini ya jua,nikaacha kwenda huko kanisani ikumbukwe nilikuwa mzee wa kanisa,niliamua kuacha kabisa ili kuendelea kutunza utu wangu maana jambo walilokusudia sikuwah kabisa kuingia kwenye mahusiano mengine zaidi ya upendo nilokuwa nao kwa mke wangu....baada ya mwaka mmoja nikiwa nimehama kanisa mke wangu bila aibu nae kahamia huko ninaposali mimi mpaka mda huu nashindwa kujua msimamo wake Ulikuwa ni upi na sijawahi kumuuliza wala kuongelea hiyo habari juu yake..
Zaidi nimejifunza kuwa mvumilivu wamkila lenye kuvuma kuwa lina mwisho wako... Niwatakie Christmas njema wapendeni wake zenu japo wanamapungufu mengi jifanye kua zile funguo ulizofungia hilo agano zimeshapote so hakuna jinsi nyingine zaidi ya kuendelea na maisha.
Mke wangu alivojikuta anavuruga ndoa yetu akijua anaimarisha ndoa yetu..
Reviewed by Love Psychologist
on
March 08, 2019
Rating:
No comments: