Sponsor

banner image

recent posts

MMMMMH WANAWAKE HAPA HAMNA KUCHOMOKA

Related image

Umeongea na yeye kwa masaa na ukatumia mbinu murua mpaka akakupatia namba yake ya simu.

Siku ya pili umeanza kuchat naye mpaka umemzoea, amekuzoea.

Imepita siku kadhaa bado mnatumiana jumbe fupi lakini inafika mahali flani unaona kama gemu yako inaenda kimtindo ambao hautarajii.

Unajaribu kutumia mbinu nyingine za kijanja lakini unaona kama jumbe zenu zinafifia.

Leo tumeamua kukuletea baadhi ya SMS unafaa kumtumia mwanamke kuyafanya maongezi yenu yawe ya kuvutia. Mwanzo nimekuchagulia baadhi ya SMS ambazo huzitumia binafsi wakati ambapo nacheza na jumbe kwa wanawake.

Zama nami.

SMS za kumtumia dem ili akupende zaidi

1. Ok tuseme unayechat na yeye ameangusha mstari wa kuchekesha. Badala ya wewe kujibu 'hahahah', unaweza kumjibu hivi:
Hahah! Njoo kwangu hii wikendi. Mimi ntaleta chakula wewe njoo na ucheshi wako.
ama
Hahah! Mbona hii wikendi tusiende kumtembelea John? Mimi ntaenda na chakula, wewe utakuja na ucheshi.

2. Kama unayemzimia umekupa fununu ya kuwa ameboeka ama akikwambia ya kuwa hajafanya jambo la kumsisimua siku nzima unaweza kumjibu hivi:
Well, nlikuwa naenda matembezi sahizi kununua ice cream na vibanzi, wataka twende pamoja?

3. Kama unayempenda amekutumia meseji akikuambia ya kuwa amekumiss, ama alitamani ungekuwa katika mkutano flani ambao hukuwepo ungemjibu hivi:
Najua napendeka. Bila shaka najua pia mimi ningejimiss kama sikujiona katika huo mkutano :-)

4. Ukigundua kama mwanamke anakupenda halafu akakutext "hello, mambo vipi?" Unafaa kumjibu kwa kumthamini kujiona kama umempa kipao mbele. Waweza kumjibu hivi.
Hello mrembo. Nimetoka kwa mazoezi sahizi/gym...waweza kunipa muda kiasi nioge kabla sijarudi?

5. Jaribu kutumia jina la unayemzimia kila baada ya sms 4-5 hivi. Utakuwa unaigonga hisia yake.
Hi Mourine, usiniambie utakosa kuhudhuria. Utakosa mengi

Mambo Pete, wasemaje?

6. Kama umeona sms ambayo imekufurahisha ama kukuchekesha, huyo mwezako hawezi kuona. Hivyo lazima umjibu kwa mtindo flani kuashiria ya kuwa umefurahishwa. Mtumie meseji ya kuzidisha jambo.
Lol. Hahah umenichekesha karibu uvunje mbavu zangu. Hivi huu ucheshi wote unautoa wapi?

7. Wakati flani inaweza kutokea unayechat naye akakueleza mambo ambayo aliweza kufanya hadi akafanikiwa. Usipoteze nafasi hii nzuri ya kutoa pongezi yako kistadi
Wow! Niseme nimependezwa ama nimependezwa na wewe....chagua moja ;-)

8. Kama mazungumzo yenu yamefikia level ya tenshen ya kimapenzi unaweza kumtext hivi
Hivi usiku huu umevalia nini?

Eti wataka kuniambia umelalia tumbo lako ama mgongo wako?

9. Kama ni sms ya kwanza ya siku jaribu kuwa mfidhuli na msukaji wakati uo huo
Hello. Kwani wewe ni nani? Ama ni yule mwanamke mrembo niliyekuwa nikichat naye jana.

10. Kubadilisha gumzo ghalfa wataki ambapo mnarushiana sms za mapenzi
Wewe: Kabla hatujaendelea na chat, kuna kitu nataka kukuambia...pole.
Mwenza: Ok, niambie hakuna shida
Wewe: Siku ya kwanza nlipokutana na wewe nilivutiwa na wewe hapo hapo ;-)

11. Unaweza kumwitisha mwanamke mtoke out bila kuifanya ionekane kama ni deti
Wewe: So kawaida siku za wiki nyakati za jioni unafanya nini?
Mwenza: Nini nini nini
Wewe: Basi kesho naona utakuwa ukifanya jambo tofauti wakati huo
Mwenza: Kitu gani kimekufanya mpaka useme hivyo?
Wewe: Sababu kesho naja kukuchukua nikutembeze ulijue jiji. Tutapumzika kwa mkahawa flani mida ya saa tatu usiku...na tafadhali usiulize maswali ya zaidi. 

12. Kama wewe na mwenza wako mnasoma ama mnafanya kazi sehemu moja unaweza kumtumia jumbe io hio siku baada ya nyinyi kufumukana.
Leo ulikuwa umevalia kunipendeza...ni ukweli ama nimekosea ;-)

Ok. Matumizi ya hizi sms zitalingana na wakati na jinsi ambavyo zinatumika. Huu ni mfano tu, unaweza kujeuza sms hizi ili zifanye kazi kwako. Usisahau kusoma machapisho ya awali tuliyoyachapisha ili unoe makali yako wakati wa kumtext mwanamke.
MMMMMH WANAWAKE HAPA HAMNA KUCHOMOKA MMMMMH WANAWAKE HAPA HAMNA KUCHOMOKA Reviewed by Love Psychologist on March 24, 2019 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.