Sponsor

banner image

recent posts

Mo J “Pamoja na Migogoro Yetu Kibao Bado Nataka Kumuoa Gigy”

Mtangazaji wa Choice Fm ambaye amezaa na msanii wa Bongo fleva Gigy Money, Mo J amefunguka na kusema kuwa pamoja na kwamba yeye na Gigy wana matatizo mengi Lakini Ndiye mwanamke anayetaka kumuoa.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers,  Mo J alisema kuwa mpango wa kumuoa Gigy Money alikuwa nao kwa muda mrefu kwa sababu kwanza ni mwanamke aliyethubutu kubeba mimba yake kwa kipindi chote cha miezi tisa hivyo kumpa heshima ya kuitwa baba.

Gigy ndiyo sababu ya mimi leo kuitwa baba, nampenda sana hayo mambo mengine ya migogoro huwa yanatokea tu kwa bahati mbaya, namshukuru Mungu Gigy ni muelewa hivyo huwa tunaongea na kumaliza tofauti zetu wenyewe, kwa hiyo Mungu akipenda kabla huu mwaka haujaisha nitafu nga naye ndoa”.

Pamoja na Mo j kusema hayo Lakini Gigy ameonekana akiwa na mwanaume mwingine na ameweka wazi kuwa amemuacha Mo J na hawezi kurudiana naye.
Mo J “Pamoja na Migogoro Yetu Kibao Bado Nataka Kumuoa Gigy” Mo J “Pamoja na Migogoro Yetu Kibao Bado Nataka Kumuoa Gigy” Reviewed by Love Psychologist on March 24, 2019 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.