Ndugu zangu leo napenda tulijadili tatizo la kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa, kwa maneno mengine ya mitaani linaitwa tatizo la kukosa nyege. Tutajadili sababu zinasababisha mwanamme kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa, madhara yanayotokana na hali hiyo na kisha kuona ni nini cha kufanya ili kuongeza hamu ya kufanya tendo la ndoa au kuongeza nyege. Bahati nzuri ni kwamba kuna mambo unayoweza kuyafanya kupunguza ukubwa wa tatizo hili au kuliondoa kabisa. Watu wengine wanamini kuwa hamu ya kufanya tendo la ndoa inapungua kadri umri wa mwanamme unavyoongezeka. Wakati ni kweli kwamba hilo huwatokea wengi, SIYO LAZIMA kwamba hamu ya kufanya mapenzi ipungue umri unapoongezeka. Kuna idadi kubwa tu ya wanaume ambao hamu yao ya kufanya tendo la ndoa imebaki vilevile hata umri wao ulipokuwa mkubwa kabisa. Kwanza tuanze kwa kutazama ukubwa wa tatizo hili.
Ukubwa Wa Tatizo La Kukosa Hamu Ya Kufanya Tendo La Ndoa
Wanaume wengi hawapenzi kulizungumzia tatizo hili waziwazi na hata wanawake pia. Pamoja na kwamba tatizo hili halijitokezi sana kwa wanaume ukilinganisha na wanawake, inakadiriwa kuwa asilimia 15 hadi 16 ya wanaume wana tatizo hili, kwa lugha nyepesi kuna mwanamme mmoja mwenye tatizo hili baina ya kila wanaume sita au saba. Idadi ya wanawake wenye tatizo hili ni mara mbili ya wanaume. Tatizo hili huwakera zaidi wanaume kuliko wanawake kwa sababu wanaume huchukulia urijali kama sehemu ya ukamilifu wa mwanamme na hunyongea wanapoona wana mapungufu kuhusu mambo ya mapenzi, tofauti kabisa na wanawake.Idadi ya wanaume wanaoridhika kuishi na tatizo hili ni ndogo sana ukilinganisha na ile ya wanawake. Hata hivyo tatizo la mwanmme kukosa hamu ya kufanya mapenzi limebainika kuwa ndilo linaloongoza katika kuleta migogoro ya unyumba kuliko matatizo mengine yote.
Mwanamme Kukosa Hamu Ya Kufanya Tendo La Ndoa. Nini Chanzo Na Tiba?
Reviewed by Love Psychologist
on
March 28, 2019
Rating:
No comments: