Sponsor

banner image

recent posts

Mwanaume kumletea mke wa mtu zawadi baada ya kujifungua imekaaje wadau? Msaada wa Haraka Tafadhali!



Kwa ufupi, mke wangu ameefanikiwa kujifungua mtoto miezi miwili imepita sasa.

Kama ilivyo kawaida wamemtembelea marafiki zake wakiwepo majirani na kumpa zawadi mbalimbali kama pongezi kwa kuleta kichanga duniani.

Kuna jambo limenishangaza kidogo, ndio maana imebidi nije mnipe japo ushauri wadau.

Baada ya kujifungua kuna mwanaume alifika nyumbani na zawadi nyingi akampa mke wangu kama pongezi. Mwanzoni nilijiuliza inakuwaje mwanaume aje peke yake kumpongeza mke wangu kwa kujifungua? Nilijikausha nkachukulia kawaida.

Juzi kati hapa nilifika nyumbani mda ambao si kawaida yangu kurudi (mchana) na sikumjulisha mke wangu kama narudi. Nilishangaa kidogo kumkuta tena yule mwanaume kaleta tena zawadi. Alishtuka sana kuniona kila sikumsemesha, nilipita moja kwa moja chumbani nikatulia kidogo nikitafakari.

Baada ya muda mchache mke wangu aliingia chumbani na kuniambia mgeni ameaga, anaondoka, nikamwitikia ila ckurudi hata kumuona.

Hii hali iliniumiza sana na kunipa maswali mengi ukizingatia kuna vitu mke wangu aliomba ninunue kwa ajili ya mtoto, Yule jamaa akaja navyo.

Wadau nishaurini, hivi inawezekana mwanaume u/a/ mtembelee mke wako nyumbani (akiwa peke yake) zaidi ya Mara moja kumpongeza mke kwa kujifungua.

Kuja mda ambao Mimi sipo na bila taarifa, then kuaga ghafla baada ya Mimi kurudi kunamaanisha Nini?

Nsaidieni jamani
Mwanaume kumletea mke wa mtu zawadi baada ya kujifungua imekaaje wadau? Msaada wa Haraka Tafadhali! Mwanaume kumletea mke wa mtu zawadi baada ya kujifungua imekaaje wadau? Msaada wa Haraka Tafadhali! Reviewed by Love Psychologist on March 20, 2019 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.