Sponsor

banner image

recent posts

Nampenda huyu dada,lakini ananikatisha tamaa!nifanyaje mie??




Habari zenu wana Udakuz
Mie nimekuwa katika kutafuta mwenzi wa maisha muda mrefu,na kuna wakati nilikata tamaa baada ya kuwa kila ninayempa proposal yangu anadai yuko na mtu wake.
Sasa,wiki mbili zilizopita nimekutana na mdada ambaye kiukweli ninampenda sana kwani ana sifa zote nitakazo mie,kwa hiyo nikaanzisha mawasiliano naye na mwisho wa siku tukapanga kukutana ili nimweleze hitaji langu.Baada ya kumweleza yangu ya moyoni,alidai yeye hataki kusikia habari ya uhusiano wa kimapenzi kwa sasa kwani AMEACHANA NA MPENZI WAKE MWEZI JANUARY 2013 baada ya kuwa katika mahusiano tangu akiwa form one.Baada ya kusikia kuwa ameachika nilifurahi sana sababu nilijua hii ndo nafasi yangu,japo alisema hataki mapenzi tena labda urafiki wa kawaida tu,mi sikuona taabu nilimwambia nimpe muda afikirie kwanza ombi langu!!
Tangu wakati huo nimekuwa nikionesha ukaribu naye sana,ikiwemo kumjari na kumpa zawadi LAKINI Amekuwa akinambia NAPOTEZA MUDA WANGU TU,
SASA Wadau,naombeni mnishauri mwenzenu nifanye nini ili huyu dada awe wangu wa maisha?Nampenda kwa moyo wangu wote na nataka aje awe mama watoto wangu!NIFANYEJE JAMANI???
Nampenda huyu dada,lakini ananikatisha tamaa!nifanyaje mie?? Nampenda huyu dada,lakini ananikatisha tamaa!nifanyaje mie?? Reviewed by Love Psychologist on March 29, 2019 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.