Kwa wanawake wengi wanapowafumania waume zao akili zao kwanza huenda katika kupambana na mwizi wao. Kwamba atatafuta namba ya mwnaamke ampigie na kumuambia aachane na mume wake, atamfuata na hata na marafiki na kumtishia na kumuambia amuachie mumewe.
Wengine hukaa kimya na kuomba msamaha kwa kufumania. Hayo ni mambo ya kihisia, kwamba ilia angalau kupunguza hasira ukimtukana mtu ambaye anatembea na mume wako basi itaisaida kidogo wewe kupungukiwa na hasira lakini hiyo haitasaidia chochote katika maisha yako.
Kwanza sio kwamba mumeo ataacha kuchepuka, hapana anaweza kubadilisha tu mwanamke au akaendelea naye na kufanya tu kwa siri, lakini anaweza hata asifanye kwa siri ikawa kumfumania ndiyo umempa tiketi ya kuchepuka kwa uhuru, si unajua bwana! Sasa najua wanawake wengi mkiwafumania wanaume zenu mtawasmehe.
Mtatafuta sababu za kiupuuzi puuzi kuwasamehe, lakini kama mume wako kafanya mambo mpaka karuhusu umfumanie basi jua kua umeshampa tiketi ya kuchepuka hivyo unapaswa kuona picha kubwa kwani anaweza kukutelekeza. Ndiyo mimi akili yangu inaelekea katika kukulinda kiuchumi zaidi.
Nikimaanisha kuwa, si ulikua unasema anakupenda, wewe ndiyo kila kitu kwake lakini kakuacha kachepuka na mwanamke mwingine. Hivyo anaweza pia kukuacha na kuoa mwingine akakutelekeza na watoto, najua huamini, kama ambavyo ulikua huamini kua atachepuka, kwa maana hiyo basi hembu jilinde kiuchumi kwa kufanya yafuatayo;
(1) Tafuta Kazi Ya Kufanya; Kama ulikua unafanya kazi basi shikilia kazi yako, anza kua siriasi na kazi yako, kua siriasi na pesa zako. Najua wanawake wengi wakiolewa huona kuwa hawahitaji kufanya kazi au hata wakifanya hutumia pesa zao kwa mambo yasiyo na msingi, sasa ukishafumania hata kama ni mara moja hiyo ni kengele.
Kama alikukataza kufanya kazi mpashe na muambie kuwa, nimeshakufumania naogopa kutelekezwa na kwenda kuwa ombaomba kwa ndugu. Muambie kama umeweza kunisaliti siku ukinitelekeza nitakua mgeni wa nani? Gombania kufanya kazi na kile unachokipata hakikisha unawekeza na kinakua na faida.
Wanawake wengi huvumilia mateso kwakua hawawezi kujihudumia kikipato. Kwamba kama ukimsamehe, anaweza asikuache lakini akazidisha wanawake, akawa anakunyanyasa na hata kukupiga. Sasa kama kazi huna huwezi kujilisha utalazimika kuvumilia. Hivyo ukishamfumania mume wako hata kama akisema kabadilika wewe fanya kazi kama “Single Woman”.
(2) Chunguza Uwekezaji Wenu Na Shiriki; Najua wanawake ni kama FBI kuchunguza mpaka kumfumania ulifanya kazi kubwa lakini tatizo mnachunguza mambo ambayo hayana maana sana na mnaacha yale ya maana. Umejua anachepuka na umemsaehe, umeumia bure lakini hujui hata hati ya nyumba kaandika jina gani.
Hujui mume mali zake ni kiasi gani, najua unajidanganya kuwa hata tukiachana tunagawana, dada yangu kama nyumba hati ina jina la Mama yake hata kama ulijenga wewe na yeye hakuchangia kitu jua si yako. Kwasabu hiyo basi ukishamfumania basi amka na anza kuchunguza mali zenu zinamilikiwa na nani na ziko wapi.
Mbali na kukuacha lakini anaweza kukutana na mchepuko mjanja, akashikiliwa nyota akapeleka kila kitu, wewe ukabaki tu unalia unamuachia Mungu wakati kashakupa akili, chunguza ujue anamiliki nini na kipo kwa jina gani, usibweteke tena na kujipa moyo kua nimezaa naye hatatelekeza wanae, anaweza!
(3) Jua Kila Kitu Kinachoendelea/Jua Zilipo Nyaraka Muhimu; Usijue tu kwamba mnamiliki nini, lakini hembu jua na mahali nyaraka zilipo, hati ya nyumba iko wapi, kama kunakiwanja hati iko wapi, vipi kadi ya gari na kila kitu. Jua biashara inaendaje na namna ya kuiendesha, fahamu zilipo nyaraka zote na mara kwa mara angalia kama kweli zipo.
Usimuamini tena tu hivyo hivyo kijinga wakati ushaona dalilia kua kuna uwezekano ukaachwa. Acha kuwa mjinga kwaufuatilia tu kua naatembea na nani, anampa nini mchepuko, angalia masalahi mapana kwani anaweza kukuumiza na kukudhulumu pia.
(4) Kua Mbahili; Dada yangu, niwakati sasa wakuacha kufanya kila kitu. Kwamba una kakazi au kabishara wewe unafanya kila kitu, unalipia ada, unalipia chakula na kila kitu. Mwanzoni ulikua hujui kuwa pesa za mumewa ko zinaenda wapi, lakini sasa Mungu kakuonyesha kua zinaenda kwa mchepuko.
Niwakati sasa na wewe kua mbahili kuacha kulipia kila kitu., kumuacha mume abebe majukumu ya mwanaume ndani ya nyumba. Pesa yako ambayo utaipata basi wekeza kivyako, ndiyo kama umemfumania na unaona kabisa hajabdilika basi acha kunyenyekea na kumlisha kila siku, no muachie majukumu ya kulea familia na jiangalie wewe.
(5) Wekeza Kivyako; Najua si kitu kizuri kuwekeza kivyako, lakini narudia kumfumaia mume wako ni ishara kua unatakiwa kujiangalia wewe pia. Kwamba nilazima uwe na kitu chako ili hata mkiachana asije kuuza kila kitu na ukaenda kuwa mzigo. Nunua ka kiwnaja na jina lako, jikusanye na fanya vitu vidogo vidogo kivyako.
Hii ni kama umemfumania lakini ndiyo kwanza anazidi, kwamba haonekani hata kujuta na anaona kama kitu cha kwaida. Lakini kuna yule aliteleza kajutia na hata kama hajaacha lakini hakuonyeshi. Huyu unaweza msamehe lakini hata mkiwekeza pamoja hakikisha jina lako lipo katika kila karatasi.
Mwisho nimalizie kwa kuwakumbusha Dada zangu kua inauma sana kusalitiwa, lakini inauma zaidi kama umechuma mali na mwanaume halafu akakuacha na kwenda kula na mwanamke mwingine. Kwamba akupotezee muda, akuzalishe na kukutelekezea watoto ulee halafu kila senti mliyochuma pamoja anachukua.
Ndiyo maana nasema kuna wakati muwe tu na akili na kusema hapana, nikianza kufuatilia michepuko yake nitachanganyikiwa, anza kufuatilia mali zake na hapa ndiyo nakuambia na wewe anza kumchuna utengeneze chako na wewe uwe huru kiuchumi. Ili hata akikutimua angalau una pakulala na wanao
NINI CHA KUFANYA UNAPOMFUMANIA MUME WAKO!
Reviewed by Love Psychologist
on
March 22, 2019
Rating:
No comments: