Sponsor

banner image

recent posts

Queen Darleen Afunguka Sakata la Kumtelekeza Baba Yao

Queen Darleen Afunguka Sakata la Kumtelekeza Baba Yao






Dada wa msanii Diamond Platnumz, Queen Darleen amesema baba yao, Mzee Abdul wanamjali na kumthamini licha ya kuwa jamii inachukulia tofauti.

Kwenye mahojiano na kipindi cha The Playlist ya Times Fm amesema wamekuwa wakimpa msaada mara kwa mara pindi inapohitajika pasipo kuzungumza kwenye vyombo vya habari.

"Huwezi ukawa kila unachompa mzazi wako utangaze, mimi nadhani mzee anatukosea kila anachokitaka anakipata na kwa wakati,’’ amesema Queen Darleen

"Kulikuwa kuna vitu tulitakiwa kumfanyia sio vizuri kuviongea, hata yeye huko aliko anajua anafanya interview anaweza akavizungumzia,’’ ameongeza.

Wiki chache zilizopita baba mzazi wa wasanii Diamond Platnumz na Queen Darleen, Mzee Abdul  alifanya mahojiano na vyombo tofauti vya habari na kuzua gumzo miongoni mwa mashabiki wa wasanii hao, wengi wakiamni mzee huyo  hana msaada wowote kutoka kwa watoto wake kutokana na kile alichokuwa akikizungumza.

Queen Darleen Afunguka Sakata la Kumtelekeza Baba Yao Queen Darleen Afunguka Sakata la Kumtelekeza Baba Yao Reviewed by Love Psychologist on March 22, 2019 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.