Kwanza ifahamike mapema ninapozungumza dalili za asiyekupenda kwa dhati, sina maana nachonganisha watu katika ndoa zao, ila kuwatanabahisha kaka zangu kugutuka katika maisha yao ya kila siku, kumekuwa na ulahai wa hali ya juu katika ndoa nyingi hapa kwetu Zanzibar na hii yote inachangiwa na ugumu wa maisha kwa ujumla.
Nitajaribu kuziweka bayana dalili za Mwanamke asiye kupenda kwa dhati lakini hii haimaaanishi kuwa ufarakano katika mapenzi yenu bali ukae na kufikiri na kuyapima kwa kina haya ninayoyaandika humu isiwe kuporotoka na kuanza mtafaruku kwa kuwa Abdullmalik kasema.
1 : Hataki kuambatana na wewe katika matembezi na kama ikiwa lazima anakuwa mtu wa masharti mara akuambie tangulia nakuja au kutembea nawe kwa mbali.
2: Anapata kigugumiza kukutambulisha kwa rafiki zake na jamaa zake.Ukimwambia tuachane,atakuambia sawa,ukimpata mke mwenzangu nionyeshe,na mimi ntakuonyesha shemeji yako.Damn women.
3: Haonyeshi kubana matumizi kwa ajili ya maendeleo, kwake ni kufuja na kwenda mbele na huwa mfujaji mkubwa wa pesa na anapokosa kununa kabisa.
4: Anaahirisha kukutana na wewe mara kwa mara, tena bila kukueleza sababu za msingi, au kukutungia uongo wa dhahiri.
5: Anapokuwa akitoa maelezo ya mwanamme amtakaye sifa zake zinakuwa hazilingani na wewe, kwa mfano atakwambia napenda mwanamme mwenye mwili mkubwa , sifa ambazo wewe huna.
6: Hacheki kwa furaha, hata kama ukimchekesha haonyeshi furaha ya moyoni, ukimwambie twende tukatembee forodhani atakujibu ''Aaah, nimechoka mie nipo nyumbani'
7: Huwa hana wivu kabisa, hudiriki hata kukushawishi uwende Disco peke yako.
8: Hasamehe na kusahau, kosa la mwaka juzi analijengea hoja.
9: Humsisimui katika mambo ya faragha.
10: Mwepesi wa kutoa kauli ya TALAKA, ''kama vipi bora kila mtu akae kivyake vyake'' tena hataki kuambiwa ukweli na anapotokea akaambiwa hujitetea kwa kumtaja mwanaume mwingine '' Mbona Al-Udii (si jina halisi) anamfanyia hili , hamfanyii hivi mkewe'':A S embarassed:
Sifa kumi za mwanamke asiyekupenda
Reviewed by Love Psychologist
on
March 24, 2019
Rating:
No comments: