Mwanamke au Mschana kukutongoza kwa uapande wao ni ngumu sana na ni asilimia chache sana wanaothubutu kufanya hivyo lakini kwa baadhi ya wanawake wanakuonyesha hisia ambazo ni lazima kama ukiwa mwanaume kamili lazima utazielewa kwamba hapa kuna mzigo wa faida.
Waschana/wanawake wengine ni lazima ahakikishe anakupata kwa vioja atakavyokufanyia hata kama unaye girlfiend wako, wasichana wanatofautiana ila wengi wao wana-share ishara tofauti
Ishara hizi zinaweza zikakusaidia kumgundua msichana anayekupenda, Mwanamke anayekupenda hatakosa kati ya hizi
1. Mnapokutana na kuongea
Msichana anayekupenda anakuwa na tabasamu unapoongea naye kama amekuzoea, ila kama hajakuzoea anapokuona gafla tabasamu hutoweka maana anakuwa na aibu. Hawezi akakuangalia machoni atakuwa anakuangalia kwa kuibia. Sikiliza sauti yake, kama anaona aibu sauti yake itakuwa ya upole/laini. anaweza akaanza kushika shika nywele zake au kuweka sawa mavazi yake.
2. Ajali za kijitakia
Anaweza akatafuta sababu yoyote ilimradi tu akushike. Anaweza akaona kitu kidogo tu au mdudu halafu anakurukia, au anakukumbatia, anaweza kuteleza makusudi au kudondosha chochote karibu au mbele yako ilimradi ateke attention yako na uiweke kwake au kukuomba msaada.
3. Anaibia kukuchunguza
Unapokuwa umetulia zako unakuta anakuangalia kwa kuibia, ukigeuka anajifanya yuko bize na mambo yake kumbe anakuchunguza taratibu.hii mara nyingi hutokea hata kama hamjazoeana na mmeonana kwa mara ya kwanza.
4. Anapenda mgusane
Mwanamke anayevutiwa na wewe mnapotembea naye mahali anapenda kushika mkono wako, au unapokutana naye anaweza kukukumbatia ili sio wote wana huu mfumo.
5. Anatafuta ukaribu
relationship-advice-for-women-1024x607.jpg
Mwanamke aliyevutiwa na wewe anapenda kuwa karibu na wewe muda wote. Mfano akiwa na marafiki zake halafu mkakutana gafla atakufuata halafu waangalie marafiki zake utakuta kama wanateta, ukiona hali hiyo kuna siri yao yeye na marafiki zake kuhusu wewe. Anapokuwa na marafiki zake akikuona anaweza akajitenga, hata kama mmeenda out pamoja na marafiki zake, utakuta yupo karibu na wewe.
6. Anapenda umjali
Anapokuwa na tatizo au anajisikia vibaya lazima akuambie, mfano mmeenda mahali kukawa na baridi hata kama si baridi sana atasema anahisi baridi ili mradi umsaidie koti lako, hata kama kuna watu hawezi kuona aibu kuvaa badala yake atajisikia vizuri anapovaa koti lako mbele za watu kwasababu anapenda kuona anajaliwa hata mbele za watu ili waone kuwa anapendwa.
7. Hawezi kuzuia tabasamu
smile.jpg
Unapomwonyeshea tabasamu lazima na yeye akuonyeshee, hata kama kuna kitu kimemwudhi atakuonyeshea tabasamu ili mradi aonyeshe umemkuta katika hali ya furaha.
8. Ishara za mwili
Anapopita mbele yako anaweza akafanya madoido mengi ambayo yatakuvutia ila kama anajiamini. Kama hajiamini anapokuona gafla anakosa amani, utamwona anashtuka gafla.
9. Anafurahishwa na vituko vyako
Mwanamke anayekupenda daima ni mwenye furaha mkiwa pamoja. Huwezi ukamboa, hata kama ukifanya kituko ambayo haichekeshi utakuta anafurahia.
10. Anakujali
Anakuwa anakujali, mfano akiona umeumia labda umejigonga, yupo radhi akuhudumie. unapokuwa naye anaweza kuuliza “unahitaji chochote? unaweza ukasema “nina kiu ngoja ninunue maji” utamsikia “nina maji, kunywa haya yangu kwanza”.basi ujue kwamba anakujali.
MUHIMU:
Unapojua hisia hizo kwa mwanamke anayekupenda au kukuzimia usiwe na papara kuanza kumfwata na kumwongelesha mambo ya ajabu,kuwa makini sana wakati utakapomfwata, msome tabia yake, anapenda nini, jitahidi kuwa mcheshi na pia zingatia haya mambo kwa kubonyeza HAPA yatakufanya uweze kwenda naye kitandani kwa muda mfupi na akaendelea kukupenda
Tambua Ishara 10 za mwanamke Anayekutaka Kimapenzi
Reviewed by Love Psychologist
on
March 17, 2019
Rating:
No comments: