Sponsor

banner image

recent posts

Una uhakika gani kuwa u mtoto wa baba'ko?



Hii ni mada nyeti, tatanishi na yenye hisia kali. Soma ielewe na changia kistaarabu.

Baada ya kupitia tafiti za hivi karibuni zilizotangazwa na kituo cha kupima DNA ambao walitangaza kuwa, imefahamika kuwa asilimia zaidi ya 60 ya vipimo vya DNA ya kutambua mzazi wa kiume (baba) zimeonyesha kuwa baba amekuwa si baba. Amebambikiwa.

Baada ya kusoma habari hiyo ya DNA, kuna visa viwili vitatu nimeshawahi kusikia na au kushuhudia kuhusu mambo ya watoto kuwa siyo wa baba zao walioaminishwa. Ntavielezea kwa uchache hapa tujadili...

Kuna kisa niliwahi kukisikia kuwa kuna mzazi ana watoto saba na wote hao si wa mumewe wa ndoa na watu wanaowafahamu wanaelewa hilo na siyo siri. Jee, huyo mume alikuwa hana mbegu na akakubaliana mkewe azae na mwanamme mwengine au ni matokeo ya kutokuwa na uaminifu ndani ya ndoa?

Kuna kisa kingine cha baba kuwa na watoto watano, wanne kati yao huwezi kabisa kuuliza, wamefanana vilivyo na baba yao (mume wa halali) lakini mmoja kati yao ametoka tofauti kabisa, si sura, si rangi, si nywele, si urefu. Tunaowafahamu hiyo familia tulisikia watu wakisema, mama alizidiwa na akachepuka na "house boy".. Ikabaki ni hadithi mpaka nilipoupata ukweli kutoka kinywani kwa mama mzazi wa huyo mtoto. Kweli Mumewe hakuwa ni baba'ke mzazi mwanawe huyo lakini wote wanamjuwa baba'ke mzazi na imetokea ilivyotokea na wakakubali matokeo. Ukipenda kufahamu kilitokea nini, uliza.

VISA vya namna hiyo vipo vingi sana, vipo vya ndani na nje ya ndoa. Nikimaanisha kuwa wapo wana ndoa wanaobambikiana na wapo wasio wana ndoa wanaobambikiana. Pia kuna ambao hawajambambikiwa ila wamekubali matokeo, kama kisa hicho cha pili au na cha kwanza pia?

Tatizo hili la kubambikiana watoto ni la muda mrefu sana. Kuna jamii au makabila huwa hawatazami baba wa mtoto ni nani, mradi kazaliwa basi wao hukubali tu, mradi wapo kwenye ndoa mtoto anakuwa ni wake na maisha yanaendelea.

Kuna makabila mengine inasemekana wakiona mwanamme mrefu na mwenye muonekano wa afya njema basi mume humuomba alale na mkewe ili wapate mbegu!

Visa hivi ni vingi sana na nikianza kuvielezea kimoja kimoja ntawatoa raha ya kujadili isipokuwa mjadala utapoendelea ntawapa kimoja kimoja.

Jee, wewe una uhakika upi kuwa ni mtoto wa baba'ko?

Jee, wanaume mnahakikisha vipi kuwa hamjabambikiwa watoto?

Jee, binafsi ulibaini kuwa ulibambikiwa baba na baada ya kufahamu ulichukulia vipi?

Jee, ni wanawake wangapi humu wanaoelewa kuwa wamebambikia watoto baba si wao na kwa sababu zipi?

Nini, kwanini, wapi, kusudi, bahati mbaya, uasherati, uzinzi, siri za majumbani, uhuni, nyege, adventure, kipato, utoto, uzee, malezi, maadili. Zote hizo zinaweza kuwa ni sababu na nyinginezo nyingi.

Hii ni mada yenye hisia kali na kutokana na takwimu hizo za asilimia zaidi ya 60, ni lazima inawahusu wengi. Tujadili kistaarabu.
Una uhakika gani kuwa u mtoto wa baba'ko? Una uhakika gani kuwa u mtoto wa baba'ko? Reviewed by Love Psychologist on March 29, 2019 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.