MATAABIKO YA KIMAISHA ANAYOPATA MSALITI BAADA YA USALITI!
MTENDWA wa usaliti hupata maumivu makali, wakati huohuo mwanzoni msaliti hukenua kwa kudhani ameshinda. Maisha hayapo hivyo!
Anayesalitiwa humwaga machozi kwa kilio cha mahangaiko ya moyo. Husahau kumshukuru Mungu. Hutamani kulipa kisasi. Hushindwa kutambua kuwa mzunguko wa maisha ya binadamu kama Maulana alivyoumba, tendo baya humrudia mtendaji mwenyewe wasaa unapotimu.
Laiti kila mmoja angejua mataabiko ambayo wasaliti hukutana nayo, kungekuwa na nafuu kubwa ya kimaisha. Idadi ya vitendo vya usaliti ingepungua.
Msaliti anapaswa kujua; Unapomsaliti mwenzio maana yake unakuwa sawa na kuyageuza maisha yake juu chini. Hilo siyo jambo dogo, kwani unaharibu mfumo wa maisha yake. Maumivu unayompa ni makubwa mno.
Katika uhusiano wa kimapenzi au ndoa, unapomsaliti mwenzio unakuwa umeingiza kaa la moto ndani ya moyo wa mwenzako. Aliwekeza upendo wake na imani kubwa, usaliti wako unamsababishia aende kuanza upya!
Wachumba wanaachana, ndoa zinavunjika. Urafiki Unavunjika, Yupo ambaye amewahi kutafsiri usaliti kama mfano wa mtu aliyetumia muda mrefu kujenga ghorofa lakini wewe unakuja kubomoa kwa siku moja.
Imani inajengwa na huchukua muda mtu kumwamini mwenzi wake kwa kiwango cha kutokuwa na shaka juu yake. Inapotokea anabaini kufanyiwa kitu tofauti na imani aliyokuwa nayo, kila kitu hubadilika. Imani yote huondoka na ni vigumu mno kumwamini tena.
Kabla ya kufika kwenye pointi ya kuchambua mateso kama siyo mataabiko ya wasaliti, tubaki kwenye swalu la msingi umewahi Kusalitiwa katika mapenzi ?
Je unaamini kua malipo ya usaliti ni hapa hapa duniani na kwa mungu ni mahesabu tuu? Tubadilike tuache kuwasaliti wanao tupenda jamani INAUMA SANA KUSALITIWA NA UNAE MPENDA.
Chagua: Kusaliti vs Kusalitiwa
Reviewed by Love Psychologist
on
April 25, 2019
Rating:
No comments: