Sponsor

banner image

recent posts

Fanya hivi baada ya Kumaliza kufanya mapenzi

Sisemi kwamba ni lazima kuyafanya haya nitakayoyaeleza leo ila yakifanywa huwa na manufaa yake na mara nyingi yanaboresha uhusiano. Kuoga pamoja


Mtakuwa ni watu wa ajabu kama mtamaliza kufanya tendo hilo kisha kila mmoja kulala na majasho yake. Wapo wasiojali katika hili na kuona kuoga au kutooga ni uamuzi wa mtu. Elewa linapokuja suala la usafi inashauriwa mkimaliza lazima muoge.Wapo wanawake ambao wakishamaliza hukimbilia kuwaandalia maji wenza wao, wakishaoga ndipo nawo huenda kuoga. Hivi unaona ugumu gani kwenda kuoga na mwenza wako?

Unaijua raha ya kuoga na huyo wako wa maisha?
Wanaofanya hivyo wanajua raha yake na wewe ambaye hujawahi, anza leo. Mmemaliza mambo yenu, chukuaneni kimahaba, elekeeni bafuni kisha ogeshaneni kimahaba.
Baada ya hapo rudini chumbani, mkishajifuta maji pandeni kitandani mkiwa wapesi. Kusifiana
Hakuna muda maalum uliotengwa kwa ajili ya wanandoa kusifiana. Hilo linaweza kufanyika wakati wowote lakini pale mnapomaliza kufanya tendo la ndoa ni lazima utakuwa na jambo zuri la kumuambia mwenza wako.

Msifie kwa utundu na ubunifu wake. Msifie pia kwa mapenzi matamu anayokupa na ikibidi mpe sifa ya uzuri wake kiasi cha kukufanya kila unapokuwa karibu yake ujisikie amani ya kupitiliza. Wapo ambao hawana kabisa kasumba ya kuwasifia wala kuwashukuru wenza wao kwa mazuri wanayofanyiwa. Yaani wao wanachukulia kila kitu poa tu bila kujali kwamba kusifiana kunanogesha mambo. Kuelekezana

Kwenye kale kamchezo, wapo ambao wanakosea, kuelekezana na kukosoana kwa wapenzi ni jambo la kawaida. Yawezekana mwenza wako alifanya kitu ambacho hakikukufurahisha wakati mkiendelea na burudani yenu, mnapomaliza mwambie lakini kwa lugha ya kimahaba na ya upole. Naamini kwa kufanya hivyo atakuelewa na kubadilika. Zungumzieni maisha

Huu ni wakati muafaka wa kujadili changamoto na malengo katika maisha yenu. Hapa akili zinakuwa zimetulia na kila mmoja anakuwa na mawazo chanya kwa mwenza wake. Jadilini mambo yenu, wekeni mikakati ya kuliboresha penzi na maisha yenu kwa ujumla. Hayo ni baadhi ya mambo ambayo mnashauriwa kuyafanya pale mnapomaliza kufanya tendo la ndoa.
Fanya hivi baada ya Kumaliza kufanya mapenzi Fanya hivi baada ya Kumaliza kufanya mapenzi Reviewed by Love Psychologist on April 08, 2019 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.