Sponsor

banner image

recent posts

"Niliumia Kuachana na Amini, Tunakuja" - Linnah

"Niliumia Kuachana na Amini, Tunakuja" - Linnah






Msanii wa Bongo Fleva, mwanadada Linnah amefunguka kuwa hakupenda kuachana na msanii Amini kwasababu alikuwa anampenda.

Linnah amesema hayo katika 'Interview' na Planet Bongo ya East Africa Radio, alipokuwa akitambulisha ngoma mpya aliyofanya pamoja na msanii huyo.

Alipoulizwa kuwa alijisikia vipi alipoachana na Amini, Linnah amesema, "kiukweli hakuna kitu kinauma kama kuachana na mtu unayempenda, mimi binafsi ninampenda Amini ndiyo maana niliumia".

"Hakuna asiyejua kuwa mimi na Amini tulikuwa wapenzi, kwahiyo watu wanaosema kuwa hivi sasa tumerudiana, hatuwezi kuwazuia kwa sababu wanapenda kutuona jinsi tulivyokuwa tukipendana", ameongeza.

Pia kuhusu uhusiano wa sasa baina ya wasanii hao ambao chimbuko lao ni THT, Linnah amesema kuwa atatafuta wakati rasmi wa kutambulisha penzi lao, lakini kwa sasa watambue tu kuwa wako pamoja na lolote linaweza kutokea.

Amini na Linnah kwa pamoja wametambulisha ngoma ya pamoja inayojulikana kama 'Nimenasa'.

Taarifa za kurejea kwa penzi la wawili hao lilianza kusambaa hivi karibuni, ikiwa ni baada ya Amini kuachana na mkewe na Linnah kuachana na baba wa mtoto wake hivi karibuni.

"Niliumia Kuachana na Amini, Tunakuja" - Linnah "Niliumia Kuachana na Amini, Tunakuja" - Linnah Reviewed by Love Psychologist on April 11, 2019 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.