Sponsor

banner image

recent posts

Mazoezi huendana na chakula, Je unajua chakula gani unatakiwa ule ili upate matokeo mazuri zaidi

Mazoezi huendana na chakula, Je unajua chakula gani unatakiwa ule ili upate matokeo mazuri zaidi?




Kuwa na mwili wa mazoezi inachukua muda na unahitaji adabu ya hali ya juu kuupata, hii inamaanisha unatakiwa uyapende mazoezi na lazima uzingatie kile unachokula ili haya mazoezi unayoyapiga yakupe matokeo mazuri zaidi.

Kiumeni.com kama kawaida imejaribu kufanya tafiti mbalimbali na kupata mchanganuo wa vyakula, mwili wako unavyovihitaji ili kufanikisha hayo mazoezi unayopiga yakupe matokeo mazuri zaidi ya kukujengea mwili na sio kuumiza kwa uzito wote huo unaoubeba...
      Sheria #1: Punguza kula vyakula vya sukari...
Tumeshasikia wote kuwa vyakula vya sukari ni adui wa mazoezi, ila tunachotaka kukwambia punguza utumiaji wa vyakula vyenye sukari na sio uviache kabisa maana sukari ni muhimu sana kwa maisha yetu, ubongo na mfumo wa fahamu unahitaji sukari ili ufanye kazi zake vizuri, kwa hio hakikisha unapunguza sio kuacha kabisa.
     Sheria #2: Kula mafuta zaidi...

Ndio, umeisoma vizuri!, kula mafuta zaidi, mafuta hayakufanyi unenepe, ila ukiwa unakula kula sana ndo kunakufanya unenepe, ukila mafuta zaidi itakusaidia kupunguza hamu ya kutamani vyakula vyenye cabohydreti(sukari) mara baada ya kupunguza milo yenye sukari, Homoni zinaitajika sana mwilini, mafuta hutumika kutengeneza homoni na kuzipa usawa na kuufanya mwili ufanye kazi kwa usahihi, na hasa yanahusika sana kwenye homoni ya testosterone ambayo ni homoni ya kujenga na kuipa uimara misuri.
          Sheria #3: Badilisha matunda kwa majani ya mboga mboga...


 Matunda yana cabohydreti(Sukari) nyingi, ila pia yana virutubisho vingine ambavyo mwili unaviitaji, ambavyo pia vinapatikana kwenye majani ya mboga mboga, hii njia inakufanya upate virutubisha vyote ila unakuwa umepunguza ulaji wa sukari au vyakura vya cabohydreti.
         Sheria #4: Achana na pombe...
Pombe inasababisha mafuta kutunzwa mwilini badala ya kutumiwa kuleta nguvu, kwa hio kama upo makini na kutaka kujenga mwili wako itakubidi uachane na pombe, mwili huacha kumeng'enya chakula kwa muda, mpaka ini itakapoitoa pombe nje. Pia pombe huumiza mwili kwa kuufanya upungukiwe na maji pamoja na kuishiwa nguvu, hushusha kiwango cha homoni ya testosterone ambayo hujenga misuli, kwahio iwapo siku ukinywa pombe, hakikisha unakunywa na soda zenye dayati.
Usisahau kushare post hii. Share facebook, twitter, Google+ n.k bila kusahau WhatsApp! Share kote wenzio nao wasome

Mazoezi huendana na chakula, Je unajua chakula gani unatakiwa ule ili upate matokeo mazuri zaidi Mazoezi huendana na chakula, Je unajua chakula gani unatakiwa ule ili upate matokeo mazuri zaidi Reviewed by Love Psychologist on April 08, 2019 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.