Sijui ni toka zamani au siku hizi mwanaume akikutongoza anataka umkubali sasa ukimkataa atajilalamisha jamani.
Mara ooh au kisa mimi sina pesa au au kisa mimi mfupi au kisa mimi sio mweupe etc etc.
Kuna rafiki yangu kanipigia story alitongozwa na albino akamkataa. Sasa yule albino anachosemea eti kakataliwa kisa yeye albino. Katumia udhaifu wake wa ualbino ili akubaliwe. Mpaka anamwambia sikupendi wewe mwanamke unaninyanyapaa kisa mimi albino. Angekua mwingine ungemkubali.
Sijajua ni wanaume wasiojiamini au ndio ujinga tu mtu anajijaza kwamba anakataliwa kwa sababu hana kitu fulani au la.
Mkitongoza haina maana tuwakubali ukikataliwa kubali tu usianze kujitoa kasoro jamani. Maana hata nikukataa sio kwamba hupati wanawake wazuri sasa kwanini ujitoe kasoro kisa mimi nimekukataa wakati hata waliokukubali wanajua wewe mfupi, mrefu sana, huna hela, kilema, una kitambi, kiokra na vitu ka hizo na bado wapo na wewe.
Msitafutie huruma kwenye mahusiano ndio kunasababisha msijiamini mkishakubaliwa.
Mwanaume ukikataliwa ni moyo tu sio mapungufu yako
Reviewed by Love Psychologist
on
April 16, 2019
Rating:
No comments: