Sponsor

banner image

recent posts

Njia mbili za uzazi wa mpango huenda ukawa huzijui



Habari za majukumu wapendwa. Niliwahi kudadisi kuhusu njia za uzazi wa mpango hususani wanazotumia wanawake kama ya vidonge, vijiti, vitanzi, na kuyapata matokeo ya walio wengi wakilalamikia madhara ya kama kubadilika kwa siku ghafla, uke kuwa na maji, tumbo kuwa kubwa mfano manyama uzembe, tumbo kuuma sana n. k. ambapo kwa wanaozihimiza hudai ni maudhi madogo madogo. 

Lakini kwa upande wa condom na utumiaji wa kalenda ikadaiwa muda mnaotakiwa mtumie kondom mwenza hajupo teyar kutumia na mnapitakiwa msile chakula cha Taifa mwenza ndio anahitaji. Ilinibid nizigeukie njia za asili walizokuwa wanatumia wamama. Ya kwanza nilikutana nayo ya kutumia majivu ya mkaa wanaotumia hii husema huchukua majivu nusu glass na kujaza maji kisha huchuja na kunywa hii hutumika ndani ya masaa 24 baada ya tendo kufanyika. Majivu haya hudaiwa kwenda kuunguza mbegu za kiume zisijirutubishe japo madhara yake bado sijadadisi kwa upande wa madaktari. 

Ya pili wachache waliniambia hutumia asprin kwa kumeza vidonge vinne kabla ya tendo la kula chakula cha Taifa kufanyika. Japo sikupata uhakika sana kwa waliotumia njia hii kwani ilikuwa ni wawili tu wanaoijua hivyo haikunipa kujiridhisha vya kutosha. Hizi nyingine kwa sababu wahusika wakubwa niliokuwa nawadadisi njia hizi mbadala ni wamama wakubwa sana kiumri wenye uelewa flani na wabibi ilikuwa wengine hunitajia baadhi ya mimea na miti nisiyoijua hivyo ikanilazimu nivitoe hivi viwili tu. 

Zoezi hili nililifanya kwa miaka miwili taratibu taratibu japo ilikuwa changamoto kwanini ninataka kujua hilo hivyo ilinilazimu kujenga ukaribu sana kwa wahusika niliotaka kuwauliza na kuweka utani mwingi ili niweze kupata ushirikiano wa taarifa.
Njia mbili za uzazi wa mpango huenda ukawa huzijui Njia mbili za uzazi wa mpango huenda ukawa huzijui Reviewed by Love Psychologist on April 01, 2019 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.