Habarini makuu.Bila shaka ni wazima wa afya. Kuna kisa kimemkuta rafiki angu mpendwa akaniomba ushauri nkaona si vibaya nkileta kwa wanajamvi hapa huenda akaokota okota ushauri utakaomsaidia.
Anasimulia. Kwa majina naitwa kyaka Kya pakano, ni muhitimu shahada ya uhandisi chuo kikuu pendwa Tanzania (UDSM).
Mnamo mwaka 2012 nlikutana na binti(feti) mrembo Sana na aliejitunza maumbile yake. Nlianzisha nae mahusiano mpaka mwaka 2017 nlipoachana nae kwa tetesi kuwa ni mshirikina. Ni habari zilizonisumbua kwa muda mrefu mpaka nlipoamua kuachana nae kwa nguvu Mana alinipenda hakuna kifani, chochote nlichohitaji hakusita kunitimizia licha ya kuwa yeye ni mdogo kiumri na darasa pia. Alijiweza kiuchumi.
Baada ya kuachana na huyu binti nkaangukia kwenye penzi zito la binti (Mary) mtoto wa mhadhiri (prof.) UDSM, Binti alinikaa Sana kichwani kiasi kwamba ilifika pahala nkaona direction kimasomo inakwenda mrama. Bahati nzuri sikudumu nae sana, 2017 December tukawa tumeachana, kwa namna nyingine nliyafurahia Yale maamuzi kwani yalinifanya nirudi darasani. Na kwa ufupi nlifanya vizuri mwaka huo wa masomo ambao ulikuwa ni wa mwisho.
Kuanzia Hapo December 2017 hadi August 2018 sikuwa na permanent relationship, nliruka ruka Sana Hadi hapo August 2018 nlipopata binti wa kimasai (osmunda) ambae kiukweli alinituliza kabisaa, nlimpa alichohitaji, Mana sijawahi kufeli kwenye hiyo sekta, binti akatua mizigo. Sasa November 2018 huyu binti aliondoka kwenda kufanya mafunzo Mana alikuwa askari JWTZ.
Wiki mbili badae Mary ambae tuliachana mwaka umepita Sasa alirudi na penzi motomoto, kwa vile nlimpenda sikusita kuvutika kwake, penzi likazaliwa upya.
Chakusikitisha zaidi osmunda ambae Yuko mafunzoni, siku nlipokuwa namuaga nlimuachia mwanangu tumboni mwake (mimba) ko yupo anahenya nae kozi. Siku chache kabla ya December feti nae anarudi nimuoe. Kiuhalisia nkimpenda binti naingiaga mazima, hiki kitu kimesababisha hawa kurudi tena.
TATIZO. Mwanamke nnaempenda zaidi ni Mary lkn ana mapungufu mengi kuwa mke pengine maisha ya kishua aliyolelewa, FETI ni mwanamke aliekamilika vyote na ni mtafutaji sana lakini mwanga, binamu yake anathibitisha hiili, osmunda nampenda kiasi lakini kashakuwa mama mtoto, na kazi yake naona atashindwa kuwapa malezi mazuri wanangu. Dilemma inakuja Nani nimuoe atakaenifaa. Anamalizia kyaka Kya pakano.
Karibuni wanajamvi. Ndugu yangu yupo kwenye msongo wa mawazo. Natanguliza shukrani.
NB: majina hayana uhalisia. Muandishi sio mtaalamu Sana na Mambo ya simulizi, alipokosea tusibeze, tumshauri kijana mwenzetu.
Njia panda: Rafiki yangu anaomba ushauri juu ya haya yaliyomkuta
Reviewed by Love Psychologist
on
April 15, 2019
Rating:
Reviewed by Love Psychologist
on
April 15, 2019
Rating:

No comments: