Sponsor

banner image

recent posts

UMESIKIA HII? : Tetesi Za Kupigwa na Kuvua Pete Zinataka Kuniharibia Lengo Langu”-Lulu Micheal Afunguka

Muigizaji wa Bongo movie mrembo Elizabeth Michael amefunguka na kuweka wazi kuwa tetesi zilizoenezwa kwenye Mitandao ya kijamii kuwa amepigwa na mchumba wake sio za kweli.

Siku chache zilizopita kuna Stori zilisambaa kwenye Mitandao ya kijamii kuwa Lulu havai pete yake ya uchumba Baada ya kutembezewa kichapo cha Hana na mchumba wake Majizzo.

Kwenye mahojiano aliyofanya jana Januari 29 katika kipindi cha Joto la Asubuhi kinachorushwa na kituo cha redio E FM, Lulu amesema habari hizo zilianza kuenea baada ya kutangaza kampeni yake ya Save my Valentine wiki iliyopita.

Suala la Mimi kuvua pete na kupigwa linalosambaa kwenye Mitandao ya kijamii ni kama kuniharibia lengo langu la #Save my valentine wala siwezi kulizungumzia na kulipa airtime”.

Lakini pia Lulu ameongeza kuwa Ameongeza kuwa utakapofika wakati sahihi atalizungumzia hilo na kwamba kwa wakati huu angependa kuendelea na kampeni yake ya kusaidia wasiojiweza.
UMESIKIA HII? : Tetesi Za Kupigwa na Kuvua Pete Zinataka Kuniharibia Lengo Langu”-Lulu Micheal Afunguka UMESIKIA HII? : Tetesi Za Kupigwa na Kuvua Pete Zinataka Kuniharibia Lengo Langu”-Lulu Micheal Afunguka Reviewed by Love Psychologist on April 29, 2019 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.