Taarifa  ikufikie hapo hapo ulipo kwamba 99.9% ya Wanawake wengi popote pale  duniani hupenda kuwa na ama Mahusiano au Kuolewa na Wanaume ambao  Kimaumbile / Kimuonekano wanafanana na Baba zao wa Kuzaa kwakuwa  Kisaikolojia Watoto wengi wa Kike huwa na Mapenzi makubwa na Baba zao  kuliko Mama zao Wazazi.
 
 Kwahiyo Mwenzangu na Mie anza Kwanza  Kujitizama kisha ukiwa unamtongoza Mwanamke fulani anza Kwanza kuulizia  Baba yake yupoje kwa mfano akikuambia kuwa ni mrefu halafu na Wewe kumbe  ni mfupi kama Ngoma / Tumba za Twanga Pepeta au ni Emolo kama siyo  Kibiriti ( mfupi Kimuonekano ) basi usipoteze muda wako Kwake kwani  hatokupenda sana sana atakuwa ' anakuchuna ' tu hadi ukome.
 
  Ukiona Mahusiano yako na Mwanamke uliyenae kila Siku ni mabaya tu anza  Kwanza kuanzia Vimo vyenu kisha Kaangalie na Kimo cha Baba yake Mzazi na  ukiona tu hamuendani basi jua ya kwamba hapo ulipo siyo mahala sahihi  Kwako. Wewe mrefu kama Mlingoti wa Vodacom halafu Baba yake Mwanamke  unayemtaka ana Kimo cha Pikipiki za Bajaji unadhani hapo kutakuwa na '  Romantic Chemistry ' kweli?
 
 Nawasilisha.
  
No comments: