Juzi nilikutana na binti mrembo maeneo ya rangi3 akanipa namba leo Ndo tulipanga kukutana katika restaurant moja apa rangi3 inaitwa taweed restaurant.
Mda wa kukutana ulipofika nikajongea cha kushangaza naona mtu anakuja na watu wake watatu kisaikolojia ukiwaangalia wamekuja kimaangamizi washamba,wachafu,mtu hata sikumtongoza washaanza kuniita shemeji mda wote wanajichekesha maskini walikuja kunikomoa kumbe mwanaume nimewanunulia vitu na ushamba wao wamekula maskin vingine wamebeba wakaondoka mmoja mmoja ndo nikabaki na rafiki yao.
Kiukweli yule binti nilimwona classic ila kwa tabia walizoonyesha marafiki zake hafai hata kupata salamu yangu siwezi kua na mashemeji of that kind sitorudia tena kutongoza uswazi nabaki na mboga saba wangu nikirudi kwangu changombe.
Hawa mabinti wa uswazi tabu sana jamani
Reviewed by Love Psychologist
on
May 03, 2019
Rating:
No comments: