Sponsor

banner image

recent posts

Kashidwa kuchagua adhabu baada ya kufumaniwa na mke wa mtu



Kuna jamaa mmoja hapa mtaani kwetu huwa anapenda sana wake za watu na hii tabia amekuwa nayo kwa muda mrefu sana,washikaji tukimshauri anatuona maboya.

Sasa kama waswahili wasemavyo kuwa za mwizi arobaini jamaa katika mishe mishe zake akazama na mke wa mshikaji mmoja gesti ya hapa mtaani kwetu, kumbe jamaa mwenye akawa ameshapata ramani nzima kuwa jamaa anaenda kumaliza mke wake.

Mshikaji wetu akazama na mke wa jamaa kama walivyopanga,aise kumbe mwenye mke alijipanga kufanya fumanizi jamaa mwenye mke akachukua rafiki zake huko sijui aliwatoa wapi wakamtimbia mshikaji wetu gesti na kweli wakamkuta jamaa anataka kuanza shughuli wakamkamata mshikaji wetu wakamfunga kama alivyozaliwa wakamwambia achague adhabu mojawapo kati ya zifuatazo;

1. Kukatwa mashine (kiungo cha uzazi)
2. Kutobolewa macho
3. Kufunuliwa marinda,(mapenzi kinyume na maumbile) na njemba hizo zote alizokuja nazo jamaa.

Ila nasikia mshikaji akachagua kutobolewa macho, ninavyowapa hii information mshikaji yuko hospitali mahututi pia amepoteza macho yake.

Sasa swali linarudi kwako ingekuwa wewe ungechagua adhabu gani kati ya hizo tatu?
Kashidwa kuchagua adhabu baada ya kufumaniwa na mke wa mtu Kashidwa kuchagua adhabu baada ya kufumaniwa na mke wa mtu Reviewed by Love Psychologist on May 03, 2019 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.