Sponsor

banner image

recent posts

Nimemfukuzia kwa miezi sita na kumkosa jumla.


Kuna binti yuko chuo second year hapa kwa makonda, nimempenda na nikatumia njia ya kawaida / naturality kwa miezi sita bila kukata tamaa nikiwa nampima ki aina .Huyu binti kwa mwezi huo nahakikisha namtumia sms kumjulia hali kila siku na nikipata chance hata kidogo tunachati tu japokuwa yeye saa zingine huchelewa kunijibu lkn akijibu tu naendelea bila kukata tamaa,na kwa wiki naenda kumjulia hali Mara moja chuoni tunakaa sehem tunapiga story, kwa huo muda wote sijawahi kumnunulia hata vocha Wala hata Senti moja sijampa kasoro siku moja aliniagiza Chakula nikiwa naenda kumjulia hali hostel nikamnunulia chips ,matunda ,juice na mazagazaga haikuzidi hata 20,000/= . Siku zote nilikuwa namwambia nampenda sio tu kumchezea bali kuwa mchumba wangu ili badae awe mke wangu akimaliza chuo.na kwa kuwa alikataa hawezi kuwa na Mimi muda huo wote eti ana mtu wake na kwa muda huo sijawai kuona dalili yoyte kuwa ana mtu .Tukawa tu marafiki wa kawida lakini nikimgusia mahusiano anakasirika ghafla na kuondoka bila hata kuniaga badae ndio anapiga simu na kunionya ili tuendele kuwa marafik nisimwambie swala la mahusiano.

Huyu binti nilimdangaya nafanya kazi kampuni flani na ninapewa chini ya laki tano ,akanishauri hiyo hela ndogo nifikirie kuexpand kipato kwa kuanzisha any bisness nilimwelewa kwa ushauri wake ,nilimwambia ukweli kuhuxu elimu yg kidato Cha sita, kwa muda huo wote nilimwambia plann yg kwake na kwa kuwa nilimpenda Kuna kipindi nilikuwa Nampa pesa kidogo lakin hachukui ananiambia ni save nianzishe bisness, Mara ya kwanza nilimpa hamsini elfu hakuchukuwa nikawa Nawaz labda ndogo ikapita Kama mwez nikampa laki moja akakataa kuchukuwa neno lake ni Lile Lile ni (save) nianzishe bisness...hapo nikasema nimepataj wife materia japokuwa hajakubali nitaenedelea kubembereza mpaka mwisho akubali .

Sasa ilifika hatua nikachoka kumbembereza coz mahusiano hataki kusikia na akisikia anakasirika ghafla, sasa mm lengo langu for relationship ni kasema hapa napoteza muda wangu wa kukaa nae badala ya kukaa kwenye kabiashar kangu huo muda wa kukaa nae niwekeze kweny bisness .Nikaanza kumpotezea lkn moyo inakataa na hata nikisema leo simpigi kumjulia hali nashangaa tu nimeshampigia ... hahaha haya mapenzi duh ..na nisipo ongea nae kazi haiendi Kama nime addicted vile .

Sasa wiki iliyopita nilikuwa kwenye maumivu makali ya mapenzi baada ya huyu binti mwanachuo kuniambia maneno makali na ikasababisha nikafunga ka ofisi kangu mapema coz nilizidiwa na maumivu ya mapenzi ...aliniambia maneno haya.

1.Hajawai kuwaza kudate au kuolewa na mtu mwenyew elimu chini yake .

2.Hawezi kuolewa na mwenye kipato chini ya laki tano japokuwa hapo nilimdangaya kuwa nimeajiriwa lakini Nina kaofisi kangu kadogo na hata kipato ni zaidi ya hapo.

3.Ana ndoto kuwa millionaire kwa hiyo anataka mtu mwenyew ideas ya business.

4.Nitafute mtu wa hadhi yangu .

5.Hana hisia na Mimi.

Baada ya hapo akaniblock kila sehemu ,ikanibid nikubali matokeo kwa maumivu hivyo hivyo , sasa leo nipo ofisini kwangu lakini sikuwa sehemu ninayonekana kwa urahisi nikamsikia sauti yake ikabidi nipige chabo kwa kuangalia kisiri... dah ni yeye wakiwa na mabest wake wawili na hawakujua hapo ndio ka ofisi kangu nikasikia wanabagain bidhaa kwa kuwa nampenda na uvumilivu ikanishinda nikajitokeza ,baada ya kuniona akanisalimia ki aina na akagairi kununua wezake tukaongea nao kikawaida baada ya hapo nikampa bidhaa bure akagoma kuchukua.Kikubwa Huyu binti nampenda na nilitaka nimtongoze kulingana na hali yangu kihalisia sikupenda nimdanganye kasoro kazi ndio nilimdangaya ili nimpime ni after money, sita fanya kosa hiyo kwa hawa viumbe ....miezi sita naambulia patupu.
Nimemfukuzia kwa miezi sita na kumkosa jumla. Nimemfukuzia kwa miezi sita na kumkosa jumla. Reviewed by Love Psychologist on May 10, 2019 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.