Sponsor

banner image

recent posts

Kisa cha Kusikitisha: Fuatilia hapa



Mimi ni binti wa miaka 27, nimeolewa na ndoa yangu ina mwaka mmoja na nusu sasa. Mimi na mume wangu tuko vizuri tatizo nikuwa mume wangu ni mbinafsia sana, hataki nifanikiwe na nikifanya kitu chochote cha maendeleo basi anajaribu namna ya kukiua ili tu niwe tegemezi kwake, pesa zenyewe hatoi, ndugu zake wakiwa na shida ananilazimisha mpaka kukopa lakini mimi ndugu zangu hata wakiume basi atasema hana pesa hata kama unaona anazo.

Sababu ya kuja kwako nikuwa, juzi mume wangu amekuja kuniambia kuwa mdogo wake anataka kwenda chuo hivyo nimchukulie mkopo na kumpa kwani yeye hana pesa. Mimi nilikataa na kumuambia kuwa siwezi kumchukulia mkopo, alikasirika na mpaka leo hatuongei, kibaya zaidi nikuwa kawaambia ndugu zake, Mama yake kanipigia simu kunilaumu kuwa eti nimeolewa lakini ni kama bado nipo kwetu.

Ameongea maneno mengi, anasema mimi ni mbinafsi na mambo mengine mwisho ananiambia kuwa hata kama nisipotoa hizo pesa mtoto wake atasoma na familia yao itafanikiwa. Sasa leo mume wangu kaja ananiambia kuwa anataka kuweka dhamana nyumba tena kw amtu ili kuchukua mkopo akamlipie ada mdogo wake, ananiambia mimi si nimekataa kumchukulia mkopo wa kazini, anasema bora kupoteza nyumba lakini si mdogo wake kubaki nyumbani.

Ni nyumba ambayo tulijenga wote na mimi nilichangia lakini hata hajali ananiambia kwakua ipo kwa jina lake ana haki ya kufanyia chochote. Kaka nimechanganyikiwa, sijui kama nichukue mkopo au nifanye nini? Mume kanuna, ndugu wananinunia na sasa hivi ni mjamzito, mimba inanisumbua lakini hakuna mtu hata mmoja anajali, naweza kuumw andani hata mtu wa kuniletea maji hamna na wakati mume yupo kutwa kucha kushinda na kukesha kwa ndugu zake, niko njia panda nichukue mkopo au nifanye nini?
Kisa cha Kusikitisha: Fuatilia hapa Kisa cha Kusikitisha: Fuatilia hapa Reviewed by Love Psychologist on March 05, 2019 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.