Habari,
Mada hii ni maalum kwa wanawake na kama wao ndiyo wahusika wakuu naomba watusaidie kuelezea kwa uwazi zaidi haya maswali hapa chini.
1. Kwanini malezi yamekuwa magumu sana kipindi hiki ambacho wanawake wengi ni wasomi walio elimika vizuri, wana vipato vizuri na kushika nyadhifa kubwa ndani ya jamii kuliko kipindi chochote kuwahi tokea duniani ???
2. Kiuhalisi: Je, unaamini kwamba ipo siku ambayo mwanamke na mwanaume watakuja kuwa sawa katika nyanja zote za kijamii, kisiasa na kiuchumi ???
3. Kuhusu dhana ya maendeleo ya mwanamke: Je, unaamini kwamba mwanamke ataonekana wa maana na kuheshimika ndani ya jamii pale ambapo atakuwa na kitu cha kushindana na mwanaume au kumfanya mwanaume aogope mfano Elimu, Pesa au Cheo ??? (Kama jibu ni Ndiyo: Je, unaamini kwamba mwanamke anaweza kuishi kwa furaha na kupata amani huku akiwa amaezungukwa na wanaume wanaomwogopa)
4. Kuhusiana na falsafa ya Feminism: Je, unaamini kwamba mwanamke ambaye ni mfuasi wa hii falsafa anaweza kuwa mama mzuri katika malezi ya watoto wa kiume ??
5. Kwanini wanawake wa kiafrika wa miaka 30 iliyopita ambao walikuwa hawajasoma sana wanasifika kwa malezi mazuri kuliko wanawake waliosoma wa kizazi hiki ?? Ushahidi wa hili ni mmomonyoko wa maadili ambao umelikumba taifa kipindi hiki.
6. Hypothetical Question: Je, siku ambayo mwanamke na mwanamume watakuwa sawa katika kila nyanja, unadhani dunia itakuwa ni mahali salama zaidi ??
7. Dini ni moja ya chanzo cha wanawake kufanyiwa ubaguzi na kukandamizwa na mwanaume. Vitabu vitakatifu kama Biblia na hata sheria za dini ya kiislamu ya baadhi ya nchi kuna sehemu hazimzungumzii vyema mwanamke au hazimuweki mwanamke katika nafasi nzuri: Je, ni kwanini wanawake wengi sana wanaendelea kushikilia hizo dini ilhali wanataka usawa na mabadiliko ndani ya jamii ??
8. Unaielewaje dhana ya "Strong Woman" or "Iron Lady" : Kati ya Oprah Winfrey, Margreth Thatcher, Cookie wa Empire, Michelle Obama, Mange Kimambi, Melinda Gates,Janet Kagame na Bikira Maria Mam wa Yesu nani ni Strong Woman or Iron Lady ?
9. Je, ni sahihi kupima nguvu za mwanamke kwa kuangalia uwezo wake wa kufanya mambo ambayo mwanaume anayafanya ??
10. Je, wewe uliyeelimika unahisi unaishi vizuri na kwa amani na mumeo, kuliko ambavyo mama yako ambaye hakuelimika sana aliishi na baba yako ?? Na je, unahisi wewe uliyeelimika umefanikiwa sana katika malezi kuliko ambavyo mama yako ambaye hakusoma sana alifanikiwa kukulea wewe ???
NB: Siyo lazima ujibu maswali yote, unaweza ukajibu hata moja tu.
Mada hii ni maalum kwa wanawake watusaidie kujibu maswali haya
Reviewed by Love Psychologist
on
March 09, 2019
Rating:
No comments: