Sponsor

banner image

recent posts

Makosa yanayofanya baada tu ya kuolewa, uchokwe



Habari za mwaka mpya wakuu.

Baada ya salamu ndefu, naomba niulize hivi kwa wadada/wamama:-
Umeshawahi kujiuliza kwanini kabla ya ndoa kunakua na mapenzi motomoto sana, lakini baada tu ya ndoa mambo hubadilika? Na yule aliyekua anakupenda na kuku-sms, na kukupigia simu siku nzima, hana muda na wewe?

Kama umejiuliza hilo, na ukaamini wanaume ndivyo walivyo, labda sijui ameshapata analotaka, au whatever.. Uko wrong!!
Tatizo hili la kuonekana wa kawaida kuliko mwanzo, ni 90% linasababishwa na mwanamke mwenyewe.
Kwanini?! Nifuatilie vizuri...

1. Wanawake wengi sana kabla ya ndoa, kwanza wana-pretend, hawawi wao halisi. Wanajifanya wanapika, wanajifanya wanajali, wanahifanya wasafi, wanajifanya wanaheshimu makubaliano, wanajifanya hawapendi starehe, wanajifanya wake wema kabisa, wanajifanya ,wanajifanya, wanajifanya...
Lakini ukweli halisi hauko hivyo, ni waongo tu.
Sisi wanaume ni wadhaifu sana kwa watu tunaowapenda, na hujikuta tunafanya chochote kwa ajili yenu.
Kwahiyo, baada ya ndoa, ukionyesha tabia tabia tofauti na zile ambazo nilivutika nazo na nikazidi kukupenda, unategemea nini sasa??!

2. Mnaishi kwa mazoea saana baada ya ndoa. Yaani mtu umeshaolewa, unahisi umemaliza kazi, mume hawezi kuwa na jipya tena. Yani wewe hujihisi huna majukumu makubwa tena juu yake.
Nawaibia siri moja, ashakum si matusi, WANAWAKE WOTE MNAKUWA WAZURI KWA WANAUME MNAPOKUA MMEVAA NGUO. Ukweli ni kuwa hamvutii sana mkiwa mmezivua. Sasa usitegemee kuwa kitandani tu ndo patanipa uhuru wa kukupenda zaidi, hamvutii sana hapo, ni hamu ya dakika 30 tu, ikiisha kuna dakika 1410 katika hiyo siku, tunahitaji kukuona ukiwa unafanya vizuri zaidi anga hzo.

Mfano, Umeamka asubuhi, hata kumuuliza mumeo "umeamkaje mume wngu?" Ni ishu, kitu ambacho ulikua unafanya kila siku katika kipindi cha mahusiano. Hili ni dogo sana, lakini linaboa.

Mume anakupigia simu, "leo kwakuwa uko nyumbani naomba unitayarishie kitu flani" unaitikia vizuri, halafu unapuuza. Unaweza kujibu baadae kuwa "nilisahau", na ukahisi ni kitu kidogo sana, lakini kinachangia saana kwakweli kuonekana wa kawaida.

3. Baada ya ndoa, wengi mnakua si wasafi tena. Hamzingatii sana usafi. Mnachukulia poa tu. Unaweza kulala pia bila kuoga!! Hatari sana. Jasho kama lote, kila muda uko busy na mambo mengine, huna time na mume. Hii ni miongoni mwa factors kubwa saana zinazopelekea kuonekana wa kawaida. Be smart.

4. Ujio wa mtoto ndio janga la kitaifa. Baada ya mwanamke kujifungua mapenzi yote anahamishia kwa mtoto. Akihisi ule uchungu wake kwa mtoto uko sawa na kwa mumewe, haiko hivyo. Ni tofauti sana. Hapa ndipo ambapo mwanamke anaweza hata kumkaripia mumewe sababu ya mtoto. Anaona ni sawa tu.
Na ndio maana ndoa nyingi zaidi zilizovunjika ni za wenye mtoto mmoja, kwa sababu wanaume wengi wanashindwa kuvumilia..

Naomba nianze mwaka na hayo kwanza, naamini yatasaidia.
Good day.

Makosa yanayofanya baada tu ya kuolewa, uchokwe Makosa yanayofanya baada tu ya kuolewa, uchokwe Reviewed by Love Psychologist on March 18, 2019 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.