Sponsor

banner image

recent posts

Mke Wangu Anunuliwa Nguo za Ndani na Mwanaume



Baada yakudakua mawasiliano ya mke wangu na kukuta Jamaa akimwambia zawadi yako ipo tayari hivyo watafutane ampatie..

Baada ya siku mbili tatu nakaona kimfuko kipo na chupi nne na brazia mbili, sikuuliza ila nikahisi hii ndio ile zawadi. Nikaamua kudakua mawasiliano yake tena.

Nikakutana tena na mawasiliano wakiulizana vip ameipenda zawadi na je zimemtosha.

Kiumweli ni zaidi ya wiki tatu sasa sijamuuliza au kuonyesha tofauti yoyote kwake, ila bado najiuliza ni sahihi kwa mwanamke tena mke wa mtu kupewa zawadi ya chupi au brazia na mwanaume tofauti na Mume/Mpenzi wake..!

Lakini pia je huyu mwanamke anaweza kuendelea kua na vigezo vya kuendelea kua mke.

Lamwisho ni mwanamke / Mwanaume anapokua anaamua kumnunulia mwenzake nguo za ndani anakua anamaanisha nini?

Natumai mawazo yenu yatanisaidia Asante.!
Mke Wangu Anunuliwa Nguo za Ndani na Mwanaume Mke Wangu Anunuliwa Nguo za Ndani na Mwanaume Reviewed by Love Psychologist on March 24, 2019 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.