Niliwahi kuandika uzi wangu wa kutafuta mwenza humu ndani, katika wengi waliokuja nikabahatika kupata kijana mmoja aliyeukuna moyo wangu,nikaona nijaribu mahusiano naye sikutaka kujiachia mazima tangu nimemkubali ni wiki tatu zimepita na bado hajaweka fedha zake kwenye pochi yangu (sex) amekuwa akinionesha upendo wa hali ya juu, .
Hana elimu kabisa ila ni mfanyabiashara aliyefanikiwa, imekuwa ni kawaida kunifuata kazini kila ambapo nikimwambia aje na kunipeleka nyumbani,neno langu limekuwa sheria kwake, sasa tatizo ni hili wiki iliyopita akaniomba anifundishe kuendesha gari ili nikiweza anipe moja nitumie kati ya machache anayomiliki.
Mwanafunzi mimi nimekuwa muoga kuingia barabarani kibaya zaidi niliparamia ukuta na gari ikabonyea akanifokea sana kiukweli iliniuma kufokewa naye kwani mpaka alinitolea tusi, ndani ya gari ukapigwa wimbo wa sisi tunakula bata wa Jay mo, nikamuomba autoe akataka kujua kwanini nikamwambia simpendi Jay mo tumegombana, akataka kujua sababu sikumwambia basi hapo ndipo tatizo likaanza amenuna hataki kuongea na mimi.
Sasa Wakuu sielewi nimekosea wapi kwenye kugonga gari au kukataa kumwambia ugomvi wangu na Jay moo ni nini!!! nakosa raha yaani mahusiano yangu mapya yavunjike ndani ya wiki tatu sina rahaa kabisa
YAMENIKUTA: Nimekosea wapi
Reviewed by Love Psychologist
on
March 24, 2019
Rating:
No comments: