CC.Bahati Mfilinge Stories
Hausigeli: Nilitega limbwata kwa mwenye nyumba likamnasa ma mwenye nyumba
Jina langu ninaitwa Vumy.
Nilikuwa dada wa kazi ( Hausigeli ) nikamtamani kimapenzi baba mwenye nyumba kwa sababu alikuwa na pesa na mali nyingi sana. Nilijua nikiwa nae kimapenzi basi shida zangu zote zitaisha.
Nikaenda kuomba ushauri kwa rafiki mmoja ambae akanielekeza kwa mganga mmoja wa kienyeji ili anipe dawa niweze kumkamata kichawi baba mwenye nyumba.
Rafiki yangu aliniambia mganga huyo ni hatari sana kwenye dawa za mapenzi na kwamba endapo nitafanikiwa kuonana nae basi huyo mwanaume nitamkamata na atafanya kila kitu ninacho kitaka.
Nilipo enda kwa mganga nikapewa dawa ya kumuwekea baba mwenye nyumba kwenye chakula anachokula .
Mganga akanipa sharti moja akaniambia, nihakikishe hicho chakula hali mtu mwingine yoyote yule isipokuwa baba mwenye nyumba na ikitokea nikivunja sharti hilo nitapata madhara makubwa sana ambayo hakutaka kuyaweka wazi.
Hilo lilikuwa sharti rahisi sana Kwangu, kwa sababu mara nyingi baba mwenye nyumba huwa anarudi usiku na huwa anakula chakula chake peke yake na mara nyingi huwa anamkuta mke wake ameshakula na amelala.
Siku hiyo usiku mama mwenye nyumba akasema hali chakula kigumu, atakunywa maziwa fresh tu ya moto.
Nikamtayarishia kama alivyo agiza wakati huo huo baba mwenye nyumba nikamuandalia ugali na nyama na maziwa mtindi na kuweka dawa niliyopewa na mganga kwenye nyama ili baba mwenye nyumba akila hiyo dawa anase na anipende.
Sijui kitu gani kilimvutia? Sijui ni harufu ya chaklula au alipatwa na njaa ghafla, mama mwenye nyumba akaniambia amekipenda hicho chakula,anaomba nimpe ale halafu baba mwenye nyumba nimuandalie chakula kingine.
Nilichanganyikiwa lakini sikuwa na jinsi zaidi ya kumpa chakula nilicho kiandaa kwa baba mwenye nyumba ambacho nilikuwa nimekiwekea limbwata ili baba mwenye nyumba anase.
Baada ya kumpa mama mwenye nyumba chakula nikaenda chooni na kumpigia simu mganga kumwambia kilicho tokea.
Nilivyo mpigia simu mganga akaniambia kwa ukali kwamba alinionya tangu mwanzo niwe makini na hiyo dawa na kuniambia nisubiri kitakacho nitokea.
Kesho yake asubuhi yule mama mwenye nyumba akaanza kuonyesha upendo na mapenzi ya hali ya juu sana Kwangu kiasi nikaogopa. Mapenzi ya mama mwenye nyumba Kwangju yalikuwa yanaongezeka saa hadi saa kiasi akawa anafanya vitu ambavyo mimi ndo natakiwa kuvifanya kama vile kuosha vyombo, kufua nguo, kupika nakadhalika.
Baada ya kama siku tatu hivi , uzalendo ukamshinda akaamua kunitamkia laivu kwamba ananipenda sana na kwamba anataka tuanzishe uhusiano wa kimapenzi.
Nilimwambia siwezi kufanya hivyo, sijawahi kufanya hivyo wala sitarajii kuwa katika mahusiano na mwanamke mwenzangu lakini wala hakuweza kunielewa.
Akaniahidi vitu vingi sana.Kunisomesha chuo, kumlea na kumsomesha mtoto wangu,kunijengea nyumba, kuninunulia gari, mashamba, viwanja, kunifungulia akaunti benki na biashara.
Vyote nikakataa na kumwambia siwezi kuwa katika mahusiano ya kimapenzi na mwanamke mwenzangu.
Nilivyo ona usumbufu umezidi nikaamua kuondoka na kurudi nyumbani kwetu kijijini Kondoa, lakini kwa kuwa alikuwa anajua natoka sehemu gani Kondoa, na namba za simu za mama angu alikuwa nazo, akanifuata hadi Kondoa na kuniomba nirudi kufanya kazi kwake.
Akanipa hela nyingi na mama angu pia akampa hela. Mimi nikamwambia kuna mambo nayamalizia kijijini Kondoa yeye arudi zake dar nitamfuata baada ya wiki moja, akakubali kwa shingo upande.
Alivyo ondoka kijijini nikamwambia mama angu siwezi kwenda kwa huyo mwanamke kwa sababu nimeambiwa ni freemason. Sikutaka mama angu ajue kitu gani kinaendelea.
Ilivyo pita wiki moja sijaenda akaanza kusumbua kwa simu, nikawa sipokei.
Akaanza kumsumbua mama angu na kumuomba anibembeleze nirudi kufanya kazi kwake.
Katika kumlainisha mama angu akawa anamtumia hela nyingi tu mpaka mama angu akahamia upande wa huyo mwanamke na kunishawishi niende kufanya nae kazi.
Kama hiyo haitoshi amemjengea nyumba mama angu kijijini na huwa anakuja kijijini kwetu linapotokea tatizo lolote la kifamilia au sherehe.
Yote hayo anayajua kwa sababu anawasiliana sana na mama angu.
Hiyo ilikuwa mwaka 2015 mwishoni lakini mpaka sasa hivi bado ananisumbua na nimeshamwambia kuwa sipo tayari kufanya upuuzi huo.
Yupo kama aliye changanyikiwa au aliye pagawa na pepo.
Amegombana na kutengana na mume wake kwa sababu yangu .
Kuna kipindi alikuwa ananipigia simu kunibembeleza niwe nae mbele ya mume wake.
Mume wake alipofariki ndugu walimzuia kushiriki kwenye mazishi kwa kumtuhumu kusababisha kifo cha mume wake.
Lakini bado ananin’gan’ania tu licha ya kumwambia mimi sipo tayari kufanya anavyo taka yeye.
Kuna kipindi nilirudi kijijini kulima ufuta na kukaa huko kwa miezi mitatu na yeye akaja kukaa kijijini na kuchukua mashamba alime ufuta lakini lengo lilikuwa kuwa karibu na mimi.
Katika kipindi chote hicho usumbufu ambao amekuwa akinipa ni mkubwa mno.
Amekuwa kama zezeta au mtu aliye pagawa hivi.
Nimejaribu kila njia ya kumkwepa huyu mama lakini imeshindikana. .
Nimemwambia si awatafute wanawake wenye tabia hizo anasema ananitaka mimi na sio mtu mwingine yoyote yule.
Nimejaribu kwenda kwa mganga alio nipa hiyo dawa na kumwambia anitenganishe na huyu mwanamke amekataa kata kata anasema huo sio utaratibu wake wa kazi na kwamba uchawi huo ni wa maisha na hauwezi kubatilishwa kwa namna yoyote ile hadi naingia kaburini.
Utaisha nguvu pindi mmoja wetu atakapo itwa na Mungu kwa hiyo nivumilie tu kwa sababu mimi ndio nilifanya uzembe.
Siwezi kuendelea kuishi katika hali ya usumbufu mkubwa kiasi hiki.
Tena mganga kaniambia halafu nina bahati kwa sababu kuna wengine huwa wanafanyaga uzembe dawa anakula baba mzazi au mtoto au kwa wanaume dawa anakula mama mzazi , mtoto au dada ambao wengi wao huishia kukimbia nchi au hata kujaribu kujiua.
Kwa hivyo nishukuru walau nina bahati.
Nimejaribu kwenda kwa waganga na waganga lakini wapi.
Imeshindikana kumzuia mwanamke huyu asiendelee kunin’gan’gania.
Nimejaribu kuombewa kote imeshindikana.
SASA NDUGU ZANGU. NINAOMBA MSAADA WENU. NITUMIE NJIA GANI ILI KUMFUNGA HUYU MAMA ASIENDELEE KUNIFUATA FUATA NA KUNIGANDA
NAOMBA USHAURI MIMI NI HOUSE GIRL,NILITEGA LIMBWATA KWA BABA MWENYE NYUMBA SASA YAMENIPATA
Reviewed by Love Psychologist
on
March 24, 2019
Rating:
No comments: