Siri 7 zitakazomfanya umpendaye kuwa na furaha siku zote
Je mpenzi wako anahitaji kuwa na wewe muda wote? Tangu nigundue siri hii nimependwa mara mbili zaidi nilivyopendwa wakati wa uchumba. Naamini baada ya kugundua na wewe kama mimi hautaamini jinsi unavyopendwa… Watu huwa na tabia yakuonyesha upendo wa juu sana kwa jinsi ya tofauti na wengine huonekana kama kutokufahamu nini humaanisha. Ingawa kila mtu hutakiwa kujua namna ya kuuyeyushamoyo wa mwenzi wake kwasababu ni hatua ya mwisho ya kumshawishi mwenzi wako.
Kwaaajili ya mke wako/rafiki yako wa kike.
1. Umshtushe mke wako siku moja na mandari (mtoko). Panga mahali pa kukutania siku za wikiendi au siku yoyote ambapo mna siku ya mapumziko. Hakikisha kuwa hana ratiba yoyote nyingine zaidi ya hiyo. Ndipo unapomwambia kuwa aambatane na wewe mwende kwenye supermarket au kitu kifananacho na hiki. Mpe muda wa kujiandaa vizuri, muda wa kuingia kwenye gari, na munaweza kubeba hata vyakula laini ama vipoza njaa. Mpeleke mwenzi wako kwenye bustani nzuuri maarufu kama beach na mwambie kuwa unampenda na ndiyo maana umeeandaa hili tukio ili kumdhihirishia ni jinsi gani unampenda.
2. Mwandikie mashairi. Na kama hii sio hobi yako pia zipo sehemu nyingi zenye mvuto. Jaribu kumsomea kitabu cha mashahiri yenye ujumbe wa kumsifia, nyimbo za upendo n.k. usirudie neno lolote kwasababu itazoeleka na atakudharau.
3. Mpikie chakula kizuri na kitamu, washa mishumaa punguza mwanga wa taa na safisha nyumba. Na atakapofika nyumbani atakosa cha kusema.
4. Shika mkono wake kila mara mnapokwenda mahali popote nje na nyumbani. Kama hili haliwezekani {kwasababu mmoja wenu amebeba mototo} hakikisha unaendeleza mawasiliano ya nje. Hii itamfanya ajisikie kuwa unajivunia ukiwa nae na kamwe huwezi kumuacha.
5. Panga ratiba ya kupiga picha. Mpe nafasi mke wako ama rafiki wako wa kike ajipambe kwaajili yako, pia chukua picha zake ambazo utaweka kwenye pochi yako, ofisini ama kwenye gari lako. Mwambie kwamba yeye ni mzuri na kuwa amepiga picha nzuri.
6. Pata muda mchache wa kwake siku moja na umwandikie neno rahisi tu “Nakupenda” na bandika popote pale. Bandika hilo neno bafuni kwenye kioo ama sehemu ambao kwa haikka ataona huo ujumbe. Hii huimarisha na kumfanya yeye kuwa wa pekee sana kwako na kukupenda sana. Na kama unahitaji kupanua wazo hili unaweza kumuachia ujumbe mtamu katika maeneo yake machache pale unapotoka.
7. Kama wewe ni mchoraji unaweza ukapata hamasa na kuchora Titanic, ukapaka rangi ama kumchora umpendaye. Utapata majibu mazuri kama amani yako imeimarishwa na kama bado mwambie kwamba huwezi kuumba kitu kizuri sana kama wewe.
Kwa mume wako/rafiki yako wa kiume.
1. Baada ya kazi ngumu za wiki, mwandikie ujumbe mzuri sana wa kurudi nyumbani. Mtumie ujumbe wa upendo wa kumsihi aje nyumbani na pia wa kumkumbusha kuwa ni muda mwafaka wa kupumzika na wewe.
2. Vaa nguo za chumbani huku ukimsubiri atoke kazini. Hii itamfanya kukupenda zaidi. Na kwa hakika atakubali jitahada zako na itamuongezea upendo kwako.
3. Kama mwezi wako anarekebisha uso wake kama kunyoa ndevu, mfanyie hilo. Weka nyimbo za upendo kwa taratibu na kwa upole mnyoe. Wewe chukua muda wako na fanya hivi atajisikia kuwa anapendwa na anajaliwa.
4. Chukua muda wako mkiangaliana machoni. Kubali na tambua uwepo wake, tambua marashi na manukato yake na joto lake. Na kama unajisikia hata kumbusu fanya hivo.
5. Jifanye kumuhitaji. Mwanaume hutamani kuonekana kuwa yeye pekee ndiye anayekulinda, hivyo mwambie kuwa hujisikii vizuri na huwa unakuwa mpweke pale anapokosekana ama unajisikia vizuri na kuwa na amani pale anapokuwepo.
6. Mkumbatie kwa ghafla. Onyo-fanya hivi pale ambapo mpo wawili tu ili kwamba asije akajisikia kuwa hayuko huru au amelazimishwa. Napendekeza fanya hivyo kwa muda wa dakika 5-6 afu mpe nafasi.
7.Mnunulie tiketi ya mpira wa miguu au mpira wa kikapu ule ambao yeye angependa kuuona. Ili kuonyesha upendo nenda nae mkashabikie timu yake kwa pamoja.
No comments: