Sponsor

banner image

recent posts

Ukaribu wa Willy Paul na Nandy wahimarika, amwagia sifa

Ukaribu wa Willy Paul na Nandy wahimarika, amwagia sifa





Baada ya mwimbaji Nandy ‘African Princess’  kufanya kolabo na Willy Paul kutokea +254 Kenya kwenye ngoma ya Njiwa ambayo iliachiwa rasmi June 27,2018 kaaika mtandao wa You Tube na kufanya vizuri ndani na nje ya nchi ya Tanzania, sasa wawili hao wanaonekana kuileta ngoma nyingine pamoja.

Kupitia ukurasa wa instagram wa  Nandy ametuonyesha kipande kifupi cha video na kuandika caption ikisema ‘Hallelujah” ambapo imetabiriwa kuwa ndio jina la ngoma inayofata na kisha akamtaja mwimbaji Willy Paul. Endapo ngoma hiyo ikitoka basi itakua ni track ya pili kutoka kwa mwimbaji Nandy na Willy Paul.

Inaelezwa kuwa ngoma hii inakuja baada ya kilio cha Willy Paul kutamani kufanya kazi tena na Nandy baada ya ngoma yao ya Njiwa kufanya vizuri huku akiwa ameshusha sifa kibao kwa mwanadada Nandy na kushukuru kwa kufanya nae project hiyo ya njiwa.

“Nandy ni mmoja wa wasanii wa kike wenye sauti Tanzania na Afrika kwa ujumla, ninafuraha kufanya nae kazi kwenye project ya njiwa, sitojali kufanya nae wimbo mwingine, kufuatia mafanikio ya njiwa sitojali kufanya nae nyingine tafadhali mwambieni sitojali kufanya nae nyingine, kama unatamani sisi kufanya wimbo mwingine basi andika neno ndio” >>>Willy Paul

Ukaribu wa Willy Paul na Nandy wahimarika, amwagia sifa Ukaribu wa Willy Paul na Nandy wahimarika, amwagia sifa Reviewed by Love Psychologist on March 29, 2019 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.